Watu 9 wamepoteza maisha katika mlipuko wa gesi mashariki mwa Algeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i82284-watu_9_wamepoteza_maisha_katika_mlipuko_wa_gesi_mashariki_mwa_algeria
Mlipuko mkubwa wa gesi uliotokea jana mashariki mwa Algreia na kusababisha jengo la ghorofa tatu kuporomoka umeua watu 9 na kujeruhi wengine 16.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Apr 08, 2022 08:36 UTC
  • Watu 9 wamepoteza maisha katika mlipuko wa gesi mashariki mwa Algeria

Mlipuko mkubwa wa gesi uliotokea jana mashariki mwa Algreia na kusababisha jengo la ghorofa tatu kuporomoka umeua watu 9 na kujeruhi wengine 16.

Wafanyakazi wa huduma za uokoaji hadi leo wameendelea kuwaokoa manusura wa mlipuko huo wa mkubwa wa gesi wakipekua hadi chini ya vifusi katika mji wa Bordj Bou Arreridj ili kuona kama kuna mtu yoyote aliyefunikwa na vifusi au aliyesalia hai. Ripoti zinasema kuwa, nyumba jirani na jengo hilo lililoporomoka kufuatia mlipuko huo wa gesi pia zimeathirika. Mlipuko huo umesababishwa na kuvuja gesi. 

Rais Abdel Majid Tebboune wa Algeria ametuma salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao. Mwezi Februari mwaka huu pia watu wanane wakiwemo watoto watatu, waliuawa baada ya kutokea mlipuko wa gesi kwenye nyumba moja katika mji wa Setif huko Algeria.  

Mlipuko huo gesi ulitokea ndani ya jengo moja katika mji wa Aïn Oulmene katika jimbo la Setif na kisha kuenea katika nyumba jirani. Kampuni ya Umeme na Gesi ya Algeria ya Somelgaz ilisema kuwa, mlipuko huo ulitokea ndani ya karakana ya kutengeneza manukato.