Baadhi ya Waislamu waanza funga ya mwezi wa Ramadhani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i8569-baadhi_ya_waislamu_waanza_funga_ya_mwezi_wa_ramadhani
Baadhi ya Waislamu kutoka pembe mbali mbali za dunia wameanza ibada ya funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 06, 2016 03:11 UTC
  • Baadhi ya Waislamu waanza funga ya mwezi wa Ramadhani

Baadhi ya Waislamu kutoka pembe mbali mbali za dunia wameanza ibada ya funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Waislamu katika nchi za Saudi Arabia, Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu, Qatar na Yemen ni miongoni mwa walioanza kutekeleza ibada hiyo tukufu hii leo. Hata hivyo ibada ya swaum katika baadhi ya nchi kama vile Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatazamiwa kuanza kesho Jumanne.

Kadhi Mkuu wa Kenya, Sheikh Ahmad Muhdhar katika kikao na waandishi wa habari hapo jana alitangaza kuwa, kwa kuwa mwezi (hilali) haukuandama katika nchi za kanda ya Afrika Mashariki na Kati hapo jana, basi leo ni Shaaban 30 na tarehe Mosi Ramadhani itakuwa kesho Jumanne.

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limewataka Waislamu nchini kutumia mwezi huu kuombea amani na utulivu. Mufti na Shekhe Mkuu wa Tanzania, Abubakar bin Zubeir amesema mwezi huu ni kama chuo ambacho kila Muislamu anatakiwa kujifunza upendo, kusameheana, kupendana na mambo yote yanayompendeza Mungu.

Ramadhani ni mwezi wa 9 kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria, mwezi wa baraka na ibada ambao ndani yake kiliteremshwa kitabu kitukufu cha Qur'ani.