Magaidi zaidi 100 wa Al-Shabaab waangamizwa Somalia
Serikali ya Somalia imetangaza kuwa magaidi zaidi ya 100 wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Al-Shabaab wameangamizwa kusini mwa nchi hiyo.

Kundi la kigaidi la al-Shabaab limeshambulia mara kwa mara wanajeshi wa serikali na wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, na limehusika pia na operesheni kadhaa za umwagaji damu katika maeneo mengine ya Afrika.
Kundi hilo la ukufurishaji limekuwa likijaribu kuipindua serikali kuu ya Somalia tangu mwaka 2007.
Al-Shabaab walifukuzwa Mogadishu na Jeshi la Somalia na vikosi vya Umoja wa Afrika mwaka 2011; hata hivyo, kundi hilo la kigaidi lingali linadhibiti maeneo mengi ya vijijini katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.../