Bahrain imeweka rekodi ya kuwa na wafungwa wengi katika Mashariki ya Kati
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i9010-bahrain_imeweka_rekodi_ya_kuwa_na_wafungwa_wengi_katika_mashariki_ya_kati
Bahrain inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wafungwa kati ya nchi za Mashariki ya Kati kulingana na idadi ya raia wote wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 11, 2016 23:59 UTC
  • Bahrain imeweka rekodi ya kuwa na wafungwa wengi katika Mashariki ya Kati

Bahrain inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wafungwa kati ya nchi za Mashariki ya Kati kulingana na idadi ya raia wote wa nchi hiyo.

Tovuti ya Mitaala ya Jela (Prison Studies) imetangaza kuwa hadi mwezi Desemba mwaka 2013 utawala wa Bahrain ulikuwa umewafunga jela raia 4,030 ambayo ni idadi kubwa zaidi katika nchi za Mashariki ya Kati kulingana na idadi ya raia wote wa nchi hiyo.

Ripoti ya tovuti hiyo imeongeza kuwa, baada ya Bahrain, tawala za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Saudi Arabia na Jordan ndizo zinazofuatia kwa kuwa na idadi kubwa ya raia wake wanaotumikia vifungo katika jela za nchi hiyo.

Kwa mujibu wa takwimu, Bahrain ina jumla ya watu wapatao milioni moja na laki tatu, ambapo sehemu kubwa ya wakaazi wa nchi hiyo ni raia wa kigeni.

Tangu mwezi Februari mwaka 2011, Bahrain imekuwa uwanja wa harakati za amani za upinzani wa wananchi wanaopinga utawala wa kifalme wa ukoo wa Aal Khalifa. Wananchi hao wanapigania uhuru, uadilifu, kuondolewa ubaguzi na kutaka kuwepo madarakani utawala uliochaguliwa na wananchi wenyewe. Hata hivyo utawala wa Aal Khalifa unatekeleza sera kandamizi za mauaji, kuwahukumu wananchi vifungo vya muda mrefu jela, kuwaweka kizuizini na hata kuwavua uraia wao.../