Watu wenye silaha washambulia mashariki mwa DRC
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i9073-watu_wenye_silaha_washambulia_mashariki_mwa_drc
Duru za kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zinasema kuwa watu wenye silaha wamefanya shambulizi dhidi ya vijiji vya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 12, 2016 22:08 UTC
  • Watu wenye silaha washambulia mashariki mwa DRC

Duru za kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zinasema kuwa watu wenye silaha wamefanya shambulizi dhidi ya vijiji vya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Shambulizi hilo lililofanywa na kundi la waasi ambalo halikujulikana mara moja lilifanyika katika kijiji cha Apinzi, kilometa 75 kusini magharibi mwa mji wa Bunia, katikati mwa mkoa wa Ituri.

Kadhalika duru za kijeshi zimeripoti kuwa, wanachama wa kundi hilo walipora mali za raia wa kijiji hicho. Gili Gotabo, kiongozi wa jumuiya ya kiraia katika eneo hilo amesema kuwa kabla ya hapo pia wabeba silaha hao ambao bado hawajajulikana, walifanya mashambulizi kadhaa katika kijiji hicho. Kamandi ya kitengo cha operesheni za jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika mkoa wa Ituri amesema kuwa, hakuna mtu aliyeuawa kwenye hujuma ya kijiji cha Apinzi na amewataka wakazi wa eneo hilo kushirikiana na askari wa serikali ili kukabiliana na wanamgambo hao.