Unicef yatahadharidha kuhusu kuendelea kwa vita barani Afrika
Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limetahadharisha kuhusu wimbi jipya la kutumiwa watoto wadogo na kuendelea vita katika nchi kadhaa za Kiafrika.
Ripoti iliyotolewa leo na UNICEF imesema kuwa, nchi kadhaa za Kiafrika zimekuwa uwanja wa kutumikishwa watoto kama askari ilhali ongezeko la ukatili na misimamo mikali katika maeneo mbalimbali duniani limedhoofisha hatua zote za kukoesha utumiaji wa watoto wadogo kama askari.
Ripoti hiyo ya UNICEF ambayo imetegemea uchunguzi wa miaka 20 iliyopita wa taasisi hiyo imesema, suala la kutumiwa watoto kama wanajeshi limekuwa kadhia kuu inayofuatiliwa na taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa na kwamba makumi ya maelfu ya watoto wanatumiwa vitani. Ripoti hiyo imesisitiza pia kwamba, karibu thuluthi moja ya askari na wanamgambo wanaopigana vita nchini Yemen ni watoto wadogo.
Kuharibiwa kwa shule nyingi za Yemen kunakofanywa na ndege za kivita za Saudi Arabia kumewalazimisha watoto kushika silaha na kulinda nchi yao.
Ripoti hiyo imesema kuwa, harakati kubwa za makundi kama Daesh, al Shabab zimetatiza juhudi za kusimamisha mwenendo wa utumiaji wa watoto katika vita.