Watoto wa Nigeria watangaza mshikamano wao na watoto wa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i96018-watoto_wa_nigeria_watangaza_mshikamano_wao_na_watoto_wa_palestina
Watoto wa Nigeria wamekusanyika katika mikoa ya Kaduna na Bauchi na kupiga nara za kuwaunga mkono na kuwatetea watoto wenzao wa Kipalestina, hasa wale wanaoishi katika eneo la Ukanda wa Gaza.
(last modified 2025-10-26T06:11:13+00:00 )
Apr 08, 2023 03:20 UTC

Watoto wa Nigeria wamekusanyika katika mikoa ya Kaduna na Bauchi na kupiga nara za kuwaunga mkono na kuwatetea watoto wenzao wa Kipalestina, hasa wale wanaoishi katika eneo la Ukanda wa Gaza.

Eneo la Ukanda wa Gaza limekumbwa na mashambulizi ya anga na mizinga ya utawala wa Kizayuni wa Israel tangu Alkhamisi iliyopita, hujuma ambayo imejibiwa na wanamapambano wa Kipalestina waliolenga kwa maroketi vitongoji vya walowezi wa Kizayuni karibu na Ukanda wa Ghaza na kukabiliana na mashambulizi ya anga ya ndege za kivita za Israel.

Shirika la habari la IranPress limeripoti kuwa, katika maandamano hayo ya Bauchi na Kaduna, watoto wa Nigeria wamepeperusha bendera za Palestina na kutangaza mshikamano wao na wenzao wa Palestina wanaoendelea kulengwa kwa mashambulizi ya Israel.

Baadhi ya watoto wa Nigeria wamemwambia mwandishi wa IranPress kwamba, "Ingawa wako mbali na Palestina, lakini wako tayari kujitolea maisha yao ili kuwasaidia na kuwatetea watoto wa Palestina."

Mtoto Aliyu Muhammad, aliyeshiriki maandamano hayo amesema: "Mwisho wa Israel umefika na vita na mapambano yetu dhidi ya utawala huu yanaendelea."

Mkusanyiko wa watoto hao wa Nigeria wa kutangaza mshikamano wao na watoto wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza umefanyika wiki moja kabla ya maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds.

Ikumbukwe kuwa, katika siku za hivi karibuni, jeshi la Israel limezidisha mashambulizi yake dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa na waumini wa Kipalestina, jambo ambalo limekabiliwa na jibu la makombora la wanamapambano wa Palestina.

Muqawama wa Palestina umesisitiza kuwa Msikiti wa Al-Aqsa ni mstari mwekundu, na kwamba mashambulizi yoyote dhidi ya eneo hilo takatifu yatakabiliwa na jibu kali.