-
Kufanyishwa kazi watoto Sudan Kusini kwafikia viwango vya kutisha
Oct 26, 2025 01:14Ripoti iliyotolewa na serikali ya Sudan Kusini kwa ushirikiano na Save the Children imefichua kwamba takriban 64% ya watoto wa Sudan Kusini wenye umri wa kati ya miaka 5 na 17 wanahusika katika aina mbaya zaidi za ajira kwa watoto, ikiwa ni pamoja na ajira ya kulazimishwa, ukatili wa kingono, wizi, na kuhusika katika migogoro ya silaha.
-
Serikali ya Tanzania yasikitishwa na ripoti ya Amnesty International kuhusu madai ya kukandamiza haki za binadamu
Oct 26, 2025 00:39Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeeleza kusikitishwa kwake na chapisho la shirika la Amnesty International lenye kichwa cha habari 'Wimbi la Ugaidi' Laikumba Tanzania Kabla ya Kura ya 2025".
-
Madagascar yamvua uraia aliyekuwa rais wa nchi hiyo Rajoelina
Oct 25, 2025 11:21Rais wa zamani wa Madagascar, Andry Rajoelina, amevuliwa uraia wake baada ya kuikimbia nchi hiyo mapema mwezi huu kufuatia maandamano makubwa yaliyoongozwa na vijana dhidi ya utawala wake.
-
Rais wa Nigeria ateua makamanda wapya wa kijeshi baada ya njama ya mapinduzi
Oct 25, 2025 09:20Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, ameteua makamanda wapya wa kijeshi Ijumaa katika mabadiliko makubwa, wiki chache baada ya maafisa 16 wa kijeshi kukamatwa kwa tuhuma za kupanga mapinduzi ya kijeshi, hatua iliyosababisha pia mamlaka kufuta sherehe za Siku ya Uhuru za nchi hiyo zilizopangwa kufanyika Oktoba 1.
-
Watu wa Ivory Coast washiriki katika uchaguzi wa urais huku kukiwa na mvutano wa kisiasa
Oct 25, 2025 09:16Wapiga kura nchini Ivory Coast wamejitokeza leo Jumamosi kushiriki katika uchaguzi wa urais, wakati mvutano wa kisiasa ukiendelea kutawala hali ya taifa.
-
Zaidi ya watu milioni 30 wanahitaji misaada ya kibinadamu Sudan
Oct 25, 2025 01:50Sudan imekumbwa na moja ya mambo ya dharura mno ya kibinadamu duniani. Zaidi ya watu milioni 30 wanahitaji msaada wa kibinadamu, ikiwa ni pamoja na zaidi ya watu milioni 9.6 wakimbizi wa ndani wakiwemo karibu watoto milioni 15.
-
Jeshi la Libya lenye makao yake mashariki lakomboa raia kadhaa wa Niger
Oct 25, 2025 01:49Jeshi la Taifa la Libya (LNA) linaloongozwa na Khalifa Haftar na ambalo linadhibiti eneo la mashariki mwa Libya, lilitangaza jana Ijumaa kwamba limefanikiwa kukomboa raia kadhaa wa Niger waliokuwa wametekwa nyara na kundi moja lenye silaha la Niger tangu miezi 16 iliyopita.
-
Waangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wapelekwa Tanzania
Oct 24, 2025 23:00Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamepelekwa nchini Tanzania kwa ajili ya kusimamia zoezi la uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliopangwa kufanyika Jumatano ijayo Oktoba 29.
-
Oxfam: Zaidi ya watu milioni 21 wanahitaji msaada DRC
Oct 24, 2025 23:00Shirika la kimataifa la Oxfam limetangaza kuwa, zaidi ya watu milioni 21 wanahitaji msaada wa kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hii ikiwa idadi ya karibu humusi moja ya watu.
-
Rais Ruto asema miswada aliyosaini siku ya kifo cha Raila inalinda watoto
Oct 24, 2025 06:40Rais wa Kenya, William Ruto, ametetea hatua yake ya kusaini miswada minane kuwa sheria mnamo Oktoba 15, 2025—siku hiyo hiyo ambayo taifa lilipokea taarifa za kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu, Raila Odinga.