-
Carbonnier: Afrika inasumbuliwa na migogoro 50 ya silaha, ikiwakilisha 40% ya migogoro ya kimataifa
Oct 24, 2025 04:16Gilles Carbonnier, Makamu wa Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC), ameelezea masikitiko yake kuhusu uwepo wa zaidi ya migogoro 50 inayoendelea barani Afrika, ikiwakilisha takriban 40% ya migogoro ya silaha duniani.
-
Baraza la Utawala Sudan: Hakuna mazungumzo na RSF huko Washington
Oct 24, 2025 04:14Baraza la utawala wa Mpito la Sudan limekanusha madai ya kuwepo mazungumzo yoyote ya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwa moja na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) huko Washington, kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
-
Makumi ya waasi wauawa katika mashambulizi ya jeshi mashariki mwa Nigeria
Oct 24, 2025 04:14Jeshi la Nigeria limetangaza kwamba limewaua wanamgambo 50 waliokuwa wakiendesha shughuli zao katika makundi yenye msimamo mkali ambao walikuwa wametumia ndege zisizo na rubani kufanya mashambulizi kadhaa kwenye kambi za kijeshi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
-
Matokeo ya uchaguzi wa rais wa Cameroon kutangazwa Jumatatu
Oct 23, 2025 23:25Baraza la Katiba la Cameroon linasema kuwa litatangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa rais siku ya Jumatatu tarehe 27 Oktoba, saa 11 asubuhi kwa saa za huko.
-
Je, kujenga vinu vya nyuklia kutaiwezesha Afrika au kutaimarisha utegemezi wa kigeni?
Oct 23, 2025 07:44Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed mwezi uliopita alitangaza mipango ya kujenga vinu vya kwanza vya nyuklia nchini humo na hivyo kuashiria hamu kubwa ya bara la Afrika ya kumiliki nishati ya atomiki. Nchi za bara la Afrika zinahitaji kukidhi mahitaji ya nishati yanayoongezeka kila siku na kupunguza utegemezi wa nishati ya kisukuku.
-
Wanamgambo wa RSF waushambulia Uwanja wa Ndege wa Khartoum kwa siku ya tatu mtawalia
Oct 23, 2025 07:32Wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) leo wamefanya wimbi la mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (droni) katika Uwanja wa Ndege wa Khartoum kwa siku ya tatu mtawalia.
-
Jiji la Nairobi katika hatari ya kusombwa na mafuriko
Oct 23, 2025 02:49Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini Kenya imetoa onyo la mvua kubwa, katika maeneo kadhaa ya nchi, huku jiji la Nairobi likitajwa kuwa miongoni mwa maeneo yaliyo katika hatari kubwa ya kusombwa na mafuriko.
-
Wahamiaji karibu 40 wapoteza maisha baada ya boti kupinduka katika pwani ya Tunisia
Oct 23, 2025 02:15Afisa mmoja wa serikali ya Tunisia amesema kuwa takriban wahamiaji 40 kutoka Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara wamefariki dunia baada ya mashua yao kupinduka katika pwani ya Tunisia jana Jumatano, katika mojawapo ya ajali mbaya zaidi za meli katika eneo hilo katika mwaka huu.
-
Makumi waaga dunia katika mlipuko wa lori la mafuta nchini Nigeria
Oct 22, 2025 23:03Makumi ya watu wameripotiwa kufariki dunia katika mlipuko wa lori la mafuta nchini Nigeria. Ripoti zinasema tukio hilo limetokea katika jimbo la kati la Niger nchini Nigeria baada ya gari hilo kuteleza kutoka barabarani na kuanguka, na kumwaga mafuta.
-
Watu 46 wamefariki dunia katika ajali mbaya ya barabarani Uganda
Oct 22, 2025 09:27Polisi ya Uganda imeripoti kuwa watu 46 wamepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha mabasi mawili katika barabara kuu ya Kampala kuelekea Gulu nchini humo mapema leo Jumatano.