-
Kujitoa Imarati katika muungano wa baharini na Marekani; Sababu na ujumbe wake
Jun 03, 2023 21:55Wizara ya Mambo ya Nje ya Imarati hivi karibuni ilitoa taarifa na kutangaza kuwa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) miezi miwili iliyopita ulijitoa na kuacha kushiriki kwenye Muungano wa Nguvu ya Baharini kutokana na tathmini yake endelevu ya ushirikiano mzuri wa usalama na washirika wake wote.
-
Kuchukizwa maadui na ushindi wa kidiplomasia wa Iran katika Umoja wa Mataifa
Jun 03, 2023 06:50Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Alhamisi iliyopita iliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la 78 la Umoja wa Mataifa na vile vile ripota wa Kamati ya Upokonyaji na Kuzuia Usambazaji Silaha ya Baraza Kuu na pia kuwa mjumbe wa bodi ya uongozi ya kamati hiyo.
-
Upinzani mkubwa dhidi ya uingiliaji wa London katika masuala ya Waislamu
Jun 02, 2023 22:00Idadi kubwa ya Waislamu wamekusanyika mbele ya Kituo cha Kiislamu mjini London wakipinga uingiliaji wa serikali ya Uingereza katika masuala ya Waislamu na kuwekewa mkurugenzi asiye Muislamu kusimamia masuala ya kituo hicho cha ibada.
-
Mabadiliko ya lugha ya Russia baada ya shambulio la ndege zisizo na rubani huko Moscow: Wanasiasa wa Uingereza sasa ni walengwa halali wa kijeshi
Jun 02, 2023 08:50Ingawa mashambulio ya hivi karibuni ya ndege zisizo na rubani za Ukraine dhidi ya Moscow hayakusababisha uharibifu mkubwa, lakini lilikuwa la kwanza la kijeshi dhidi ya mji mkuu wa Russia kutoka nje ya mipaka ya nchi hiyo katika miezi kumi na sita ya mzozo wa vita vya Ukraine.
-
Luteka ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni, kuendelea kutumia turufu iliyofeli kutatua mgogoro wa ndani
Jun 01, 2023 22:15Baraza la Mawaziri la waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu linaendelea kutumia turufu iliyofeli ya kijeshi kujaribu kutatua mgogoro wa ndani unaoikabili serikali ya genge lenye misimamo mikali ya kufurutu mipaka la Kizayuni.
-
Kutishiwa kuwekewa vikwazo Uganda, njama za Marekani za kuzitwisha ufuska nchi za Afrika
Jun 01, 2023 08:42Rais wa Marekani, Joe Biden amelaani sheria mpya iliyotiwa saini na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda dhidi ya vitendo vya ushoga na kusema kuwa Marekani inaweza kuiwekea Uganda vikwazo na ameitaka Uganda kufuta mara moja sheria hiyo.
-
Onyo kuhusu kudorora Ulaya katika mfumo unaotawaliwa na Marekani
May 31, 2023 21:52Mwanafikra mashuhuri wa Marekani Noam Chomsky ameonya kwamba huenda Ulaya ikadhoofika sana kiviwanda ikiwa itaendelea kuwa chini ya utawala wa Marekani.
-
Nafasi ya BRICS duniani na umuhimu wake kwa Iran
May 31, 2023 02:20Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran atasafiri hivi karibuni kuelekea Cape Town, Afrika Kusini, kwa ajili ya kushiriki katika mkutano ujao wa BRICS .
-
Onyo la Pakistan kwa kundi la Taliban la Afghanistan
May 30, 2023 21:49Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Pakistan ameionya serikali ya wanamgambo wa Taliban wa Afghanistan kuhusiana na shambulio lolote dhidi ya ardhi ya Pakistan.
-
Msimamo wa Kiongozi Muadhamu kuhusu kuhuishwa uhusiano wa Iran na Misri
May 30, 2023 06:43Jumatatu ya jana tarehe 29 Mei, Sultan Haitham bin Tariq Aal Saeed wa Oman alikutana na kufanya mazungumzo hapa mjini Tehran na Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.