-
Moscow yasisitiza: Marekani inashiriki moja kwa moja katika vita vya Ukraine
May 08, 2022 21:57Vyacheslav Volodin, mkuu wa Duma ya Russia, ameandika kwenye mtandao wa Telegram kwamba Merekani inashiriki moja kwa moja katika operesheni za kijeshi za Ukraine.
-
Marekani; chanzo cha kusita kwa muda mrefu mazungumzo ya Vienna
May 08, 2022 06:29Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mazungumzo ya simu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuwa, sera ghalati za mashinikizo ya kiwango cha juu za Marekani ndio sababu ya hali ya sasa ya mambo inayoshuhudiwa katika mazungumzo ya Vienna.
-
Indhari ya Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro mkubwa wa chakula Afrika
May 07, 2022 22:13Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa kupanda pakubwa bei ya chakula na mafuta kutokana na vita vya Ukraine, kumeibua mgogoro mkubwa wa chakula barani Afrika ambao haujawahi kushuhudiwa.
-
Shambulio dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa, jibu huko Tel Aviv
May 07, 2022 03:37Kufuatia wito uliotolewa na walowezi wenye misimamo mikali ya Kiyahudi wa kushambuliwa Msikiti wa Al-Aqsa katika siku ya kumbukumbu ya kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina na kutangazwa dola haramu la Israel, Wapalestina wametekeleza oparesheni nyingine katika kitongoji cha walowezi hao cha El'ad huko Mashariki mwa Tel Aviv. Wazayuni watatu wameuawa na wengine wanne wamejeruhiwa.
-
Indhari kuhusu hali mbaya ya kibinadamu Afghanistan
May 06, 2022 20:48Ofisi ya Mkaguzi Mkuu Maalumu wa Marekani kwa ajili ya ujenzi mpya wa Afghanistan (SIGAR) imetahadharisha kuhusu taathira za hali mbaya ya kibinadamu nchini humo.
-
Jitihada za Iran na Uturuki kwa ajili ya kuitisha mkutano wa Baraza Kuu la Ushirikiano wa Kistratejia
May 06, 2022 03:08Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na mwenzake wa Uturuki wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu kuhusu uhusiano wa pande mbili sambamba na kujadili masuala mbalimbali ya kikanada na kimataifa.
-
Kuongezeka upinzani barani Ulaya dhidi ya kuwekewa vikwazo vya mafuta Russia
May 05, 2022 22:07Licha ya vitisho vya Umoja wa Ulaya kuhusiana na kuiwekea vikwazo vya mafuta Russia katika fremu ya kifurushi cha sita cha vikwazo dhidi ya nchi hiyo, lakini jambo hilo linaonekana kukabiliwa na upinzani mkali barani humo na hata baadhi ya viongozi wa Marekani kutoa onyo dhidi ya hatua hiyo.
-
Kuwa tayari Lebanon kwa ajili ya zoezi la uchaguzi wa Bunge
May 05, 2022 03:33Bassam Mawlawi, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Lebanon ametangaza kuwa, maandalizi ya lazima kwa ajili ya kuendesha zoezi la uchaguzi wa Bunge nchini humo katika muda uliopangwa yamekamilika.
-
Putin atia saini amri ya kuiwekea vikwazo vya ulipizaji kisasi kambi ya Magharibi
May 04, 2022 21:45Ikulu ya Kremlin imetangaza Jumanne kuwa, Rais Vladimir Putin wa Russia ametia saini amri ya kukabiliana na 'hatua zisizo za kirafiki za baadhi ya nchi za kigeni na mashirika ya kimataifa." Dikrii hiyo inasisitiza hatua za kulipiza kisasi dhidi ya nchi ambazo zimetajwa kuwa 'zisizo za kirafiki'. Kwa mujibu wa amri hiyo Russia itaziwekea vikwazo baadhi ya nchi na taasisi za kimataifa.
-
Iran yakosoa mahakama ya kimaonyesho na isiyo ya uadilifu katika kesi ya Hamid Nouri nchini Sweden
May 04, 2022 04:00Kazem Gharibabadi Katibu wa Baraza Kuu la Haki za Binadamu la Iran amekosoa kesi dhidi ya afisa wa zamani wa Iran ambaye anatuhumiwa Sweden kuwa eti amekiuka haki za binadamu na kuitaja kesi hiyo kuwa iliyo kinyume cha sheria na isiyo na uadilifu.