Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kuhusiana na uamuzi wa serikali ya Australia wa kupunguza kiwango cha uhusiano wa kidiplomasia na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i130078-taarifa_ya_wizara_ya_mambo_ya_nje_ya_iran_kuhusiana_na_uamuzi_wa_serikali_ya_australia_wa_kupunguza_kiwango_cha_uhusiano_wa_kidiplomasia_na_iran
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imechapisha taarifa ikiutaja uamuzi wa serikali ya Australia wa kupunguza kiwango cha uhusiano wa kidiplomasia na Iran kuwa kinyume na utamaduni wa uhusiano mkongwe wa nchi hizi mbili.
(last modified 2025-08-27T12:55:15+00:00 )
Aug 27, 2025 12:53 UTC
  • Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kuhusiana na uamuzi wa serikali ya Australia wa kupunguza kiwango cha uhusiano wa kidiplomasia na Iran

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imechapisha taarifa ikiutaja uamuzi wa serikali ya Australia wa kupunguza kiwango cha uhusiano wa kidiplomasia na Iran kuwa kinyume na utamaduni wa uhusiano mkongwe wa nchi hizi mbili.

Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema: "Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaeleza masikitiko yake kuhusu suala hili na inalichukulia ombi la serikali ya Australia la kutaka balozi na wanadiplomasia kadhaa wa Iran waondoke nchini humo kuwa halina uhalali wa kisheria na ni kinyume cha uhusiano wa jadi wa kidiplomasia baina ya nchi mbili." Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran inakanusha kikamilifu tuhuma zilizotolewa dhidi ya Iran kuwa inachochea chuki dhidi ya Mayahudi na kuitaka serikali ya Australia izingatie ukweli wa kihistoria kwamba suala zima la chuki dhidi ya Uyahudi kimsingi ni jambo lililoanzia Ulaya na nchi za Magharibi ambalo limejitokeza katika nchi hizo kwa namna na nyakati tofauti. Pamoja na hayo, katika miaka ya hivi karibuni, suala hili limekuwa likitumika vibaya kwa ajili ya kukandamiza maandamano yoyote dhidi ya uvamizi, ubaguzi wa rangi na mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina.