Jeshi la Israel limeua na kujeruhi makumi ya wakazi wa Khan Yunis kusini mwa Gaza + Video
(last modified Sat, 13 Jul 2024 11:48:28 GMT )
Jul 13, 2024 11:48 UTC

Ndege za kivita za jeshi la utawala katili wa Israel limeushambulia mji wa Khan Yunis kusini mwa Ukanda wa Gaza na kuuwa wakazi wa mji huo wasiopungua 71 na kujeruhi wengine 289 hadi hivi sasa.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, jeshi la utawala wa Kizayuni leo Jumamosi katika kuendeleza mashambulizi na mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya wakazi wa Kipalestina wa Ukanda wa Gaza limeshambulia mtaa wa al Rashid na maeneo ya pambizon mwa Chuo Kikuu cha al Aqsa katika mji wa Khan Yunis kusini mwa Ukanda wa Gaza na kuwauwa shahidi watu wasiopungua 71 na kujeruhi wengine 289 hadi tunaripoti habari hii.  

Vyombo vya habari vya Palestina vimesema kuwa idadi ya mashahidi huenda ikaongezeka. 

Habari nyingine zinasema kuwa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu imetangaza katika ripoti yake mpya kuhusu kupotea Wapalestina 6,400 wakazi wa Ukanda wa Gaza tangu kuanza vita na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni katika eneo hilo. 

Tangu kuanza vita dhidi ya Ukanda wa Gaza Oktoba 2023 hadi sasa kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu imepokea ripoti kuhusu kupotea na kutojulikana walipo watu zaidi ya 8,700, na imeshirikiana na familia 7,429 za Kipalestina kukusanya taraifa kuhusu watu hao waliopotea. 

Sarah Davies Msemaji wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu amesema kuwa kamati hiyo kila siku hupokea simu 500 hadi 2,500 na aghalabu yazo zinahusu ndugu wa familia waliopotea. 

Sarah Davies 

Utawala haramu wa Israel haujapata mafanikio yoyote katika vita dhidi ya Gaza ghairi ya kutenda jinai za kivita, maangamizi ya kizazi, uharibifu, kukiuka sheria za kimataifa, kushambulia taasisi za misaada ya kibinadamu na kuwasabababisha njaa na maradhi wakazi wa Ukanda huo baada ya kupita miezi 9 ya mashambulizi ya kikatili na mauaji yake ya kimbari dhidi ya Wapalestina. 

Tags