-
SAUTI, Serikali ya Congo-Brazzaville na UNHCR zaanza kuwarejesha kwa hiari wakimbizi 3000 wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
Oct 20, 2018 13:20Serikali ya Congo-Brazzaville kwa kushirikiana na Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, imeanzisha zoezi la kuwarejesha nyumbani wakimbizi 3000 wa Jamhuri ya Afrika ya Kati waliokimbilia nchi hiyo miaka kadhaa iliyopita.
-
SAUTI, mafunzo ya ndoa yaanza kutolewa Zanzibar ili kuzilinda Ndoa/ wakazi Wete Pemba, wazuia vazi la niqabu kuzuia uhalifu
Oct 19, 2018 12:27Siku chache baada ya kufunguliwa chuo cha mafunzo ya ndoa, Jumuiya ya Maimamu JUMAZA, imeanzisha program ya kutoa mafunzo hayo ili kunusuru ndoa katika jamii.
-
SAUTI, Wagombea wa upinzani Kongo DR: Serikali inafanya upendeleo wa kisiasa, imetunyima ulinzi wa askari
Oct 19, 2018 11:48Wagongea wa upinzani wa kiti cha urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wameilalamikia serikali ya nchi hiyo kwa kukataa kuwapatia ulinzi ili waweze kuendesha shughuli zao za kisiasa kwa amani kuelekea uchaguzi wa mwezi Disemba mwaka huu.
-
Kiongozi Muadhamu: Kutoa taswira ghalati kuhusu hali ya Iran, ajenda kuu ya adui + Video
Oct 18, 2018 04:36Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu jana asubuhi alionana na takriban vijana bora elfu mbili wenye vipaji na vipawa tofauti vya kielimu na kusisitiza kuwa, juhudi na kazi za makumi ya maelfu ya watu wenye vipaji katika kona zote za Iran zinachora taswira inayoleta matumaini na kuonesha hali halisi ilivyo humu nchini.
-
SAUTI, Ongezeko la talaka laifanya Jumuiya ya Maimamu Zanzibar JUMAZA kuzindua chuo cha maadili ya ndoa
Oct 16, 2018 15:02Kufuatia ongezeko la talaka kati ya wanandoa katika jamii visiwani Zanzibar, Jumuiya ya Maimamu JUMAZA imezindua chuo cha maadili ya ndoa na mtaala wake ambacho kitakuwa na jukumu la kutoa mafunzo bora ili kupunguza ongezeko hilo.
-
SAUTI, Waliohusika na mauaji ya kimbari ya 1994 nchini Rwanda sasa kuanza kusakwa kwa udi na uvumba
Oct 16, 2018 14:33Bunge la Rwanda limeanzisha zoezi la kuihoji tume ya taifa ya nchi hiyo inayoshughulikia faili la mauaji ya kimbari ya 1994, juu ya idadi kubwa ya watu waliokutikana na hatia ya mauaji hayo na kukwepa mkono wa sheria.
-
SAUTI, Serikali ya Kongo DR yakasirishwa na kitendo cha Angola kuwafurusha kama wanyama Wakongomani
Oct 16, 2018 14:29Kufuatia hatua ya serikali ya Angola kuwatimua makumi ya maelfu ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa lengo la kutaka kusafisha sekta ya madini ya alimasi kutokana na uwepo wa Wakongomani, serikali ya Kinshasa imekasirishwa na suala hilo.
-
Kesi za uchaguzi Cameroon kuanza kusikilizwa leo Jumanne + Sauti
Oct 15, 2018 23:50Tume ya Uchaguzi ya Cameroon (ELECAM) imesema kuwa, leo Jumanne Oktoba 16, 2018 ndiyo siku ya kusikiliza kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika hivi karibuni. Matokeo yaliyovuja ya uchaguzi wa rais yanaonesha kuwa Rais Paul Biya ameshinda uchaguzi huo wa Oktoba 7 kwa zaidi ya asilimia 71 ya kura. Mossi Mwasi na maelezo zaidi
-
Ubelgiji yakubali kuirejeshea Rwanda sehemu ya utajiri wake wa kihistoria + Sauti
Oct 15, 2018 23:31Kwa mara ya kwanza Ubelgiji imekubali kuirejeshea Rwanda baadhi ya nyaraka na turadhi za kihistoria za kabla, wakati na baada ya ukoloni. Ubelgiji ni moja ya madola ya Ulaya yaliyozikoloni kidhulma nchi za Afrika na kupora utajiri mkubwa wa nchi za bara hilo. Mwandishi wetu Sylvanus Karemera na ripoti zaidi
-
VIDEO: Boti za Kasi za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH zinavyopambana na manuwari za Marekani Ghuba ya Uajemi
Oct 14, 2018 10:47Kwa mara ya kwanza Iran imetoa video inayoonesha boti za kasi za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH zikikaribia manuwari ya kivita ya Marekani katika maji ya Ghuba ya Uajemi.