Raisi: Kutoa ruhusa ya kuchoma moto Qur'ani ni ishara ya ujinga mamboleo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i100262-raisi_kutoa_ruhusa_ya_kuchoma_moto_qur'ani_ni_ishara_ya_ujinga_mamboleo
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kutoa leseni ya kuidhalilisha na kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu ni kinyume na madai ya uhuru wa kusema na ni kielelezo cha "ujinga mamboleo".
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 24, 2023 07:38 UTC
  • Raisi: Kutoa ruhusa ya kuchoma moto Qur'ani ni ishara ya ujinga mamboleo

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kutoa leseni ya kuidhalilisha na kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu ni kinyume na madai ya uhuru wa kusema na ni kielelezo cha "ujinga mamboleo".

Sayyid Ebrahim Raisi, ameyasema hayo katika kikao cha baraza la mawaziri na kueleza kuwa, Qur'ani pamoja na mwanadamu mkamilifu ni nguzo mbili za mwongozo na uokovu wa mwanadamu. Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, kuidhinishwa vitendo vya hivi karibuni vya kuikashifu Qur'ani ni kinyume na madai ya kutetea uhuru wa kusema na kielelezo cha "ujinga mamboleo".

Raisi ameongeza kwamba, moja ya maagizo makuu ya Qur'ani Tukufu ni kupambana na ujinga wa aina zote, na kwa msingi huo wafuasi wa ujinga mamboleo wana chuki dhidi ya Qur'ani.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kutokana na wimbi la mwamko linaloenea kote duniani, itakuja siku ambapo watu wote watatambua dhamira mbaya, ovu na zisizo za kibinadamu za wale wanaoidhalilisha na kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu.

Itakumbukkwa kuwa Alkhamisi iliyopita kafiri Salwan Momika, mkazi wa Sweden alikivunjia tena heshima Kitabu Kitakatifu cha Waislamu zaidi ya bilioni mbili akipewa ulinzi na himaya kamili ya jeshi la polisi la Sweden mjini Stockholm.

Awali, Rais Ebrahim Raeisi, alitoa agizo la kutoruhusiwa balozi mpya wa Uswidi kuingia Iran hadi pale serikali ya nchi hiyo itakapochukua hatua madhubuti ya kukabiliana na ukiukaji unaoendelea wa kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu."

Waziri wa mambo ya Nje wa iran Hossein Amir Abdollahian amesema kwa mujibu wa agizo la Rais Ebrahim Raisi, Iran haitampokea balozi mpya wa Uswidi, ambaye alitarajiwa kuwasili Tehran ndani ya siku chache zijazo, na pia haitatuma balozi mpya huko Stockholm baada ya nchi hiyo kuruhusu vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur'ani.