Jul 25, 2023 07:47 UTC
  • Adimeri Kaviani: Vyombo vya majini vya Jeshi vitabeba Kombora la Abu Mahdi

Naibu Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yatalindwa katika eneo la kaskazini la Bahari ya Hindi na maji huru ya kimataifa baada ya vyombo vya jeshi kusheheniwa kwa kombora la Abu Mahdi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Adimeri Hamza Ali Kaviani, ameyasema hayo leo alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu umuhimu wa kombora la Abu Mahdi katika kuimarisha uwezo wa kivita wa jeshi hilo na akabainisha kuwa: kuongezwa kwa kombora hilo kwenye orodha ya makombora ya Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kunakamilisha nguvu za kiulinzi na uwezo wa kuzuia hujuma wa jeshi hilo.

Adimeri Kaviani ameelezea sifa maalumu lilizonazo Kombora la Abu Mahdi na kusema: "kombora hili linatoa jibu kwa tishio lolote hadi kwenye vina vya bahari kuu hususan kaskazini mwa Bahari ya Hindi ambalo ni eneo la majukumu na masuulia kwa Jeshi la Wanamaji.

Hafla ya kuunganishwa mfumo wa silaha ya kimkakati ya kombora la cruise la baharini la Abu Mahdi na vikosi vya Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC imefanyika mapema leo.

Adimeri Hamza Ali Kaviani (wa kwanza kushoto) akiwa na makamanda wa Jeshi na IRGC

Kombora la Abu Mahdi ni kombora la baharini aina ya cruise linalolenga umbali wa masafa zaidi ya kilomita 1000, ambayo yameongeza mara kadhaa ukubwa wa eneo la ulinzi wa baharini wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikilinganishwa na hapo awali na linaweza kupanua wigo wa operesheni za jeshi hilo.

Mfumo wa silaha ya kimkakati wa masafa marefu wa Abu Mahdi una kombora lenye sifa za kipekee miongoni mwa makombora ya aina hiyo duniani katika ulengaji shabaha kutokana na nguvu zake kubwa za kusababisha uharibifu na uwezo wa kupenya kwenye vizuizi vya kijiografia na mifumo ya ulinzi ya adui.

Kombora la Abu Mahdi ni kombora la kwanza la baharini la masafa marefu ambalo linatumia akili bandia (AI) katika programu zinazohusiana na ubunifu wa njia ya angani na mfumo wa uendeshaji na uongozaji; na lina uwezo wa kuvuka vizuizi vya kimaumbile na vya bandia pamoja na rada na mitambo ya ulinzi ya adui na kuweza kushambulia na kulenga shabaha kutokea pande tofauti.../

Tags