Kan'ani: Utawala wa Kizayuni wa Israel unakaribia kuzimu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i100332-kan'ani_utawala_wa_kizayuni_wa_israel_unakaribia_kuzimu
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ametuma salamu za rambirambi kwa familia za mashahidi waliouawa na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel huko Nablus, Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na kusema: Utawala bandia na wa kigaidi wa Israel unakaribia kuangamia na kutoweka.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 26, 2023 02:42 UTC
  • Nasser Kan'ani
    Nasser Kan'ani

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ametuma salamu za rambirambi kwa familia za mashahidi waliouawa na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel huko Nablus, Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na kusema: Utawala bandia na wa kigaidi wa Israel unakaribia kuangamia na kutoweka.

Katika mapigano yaliyotokea jana Jumanne mjini Nablus, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel waliwaua shahidi Wapalestina watatu na kupeleka miili yao sehemu isiyojulikana.

Mapigano hayo yalitokea katika kituo cha usalama cha utawala wa Kizayuni karibu na Mlima Gerizim huko Nablus.

Akihutubia wananchi wa Palestina na makundi ya mapambano ya ukombozi, Nasser Kan'ani ameongeza kuwa: "Damu safi ya mashahidi wenu haitapotea bure na utawala bandia, vamizi na wa kigaidi wa Israel unakaribia kuangamia."

Jumatatu wiki hii wakati wa kuidhinishwa mageuzi ya mahakama katika Bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel, Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon aliitaja siku hiyo kuwa siku mbaya zaidi kwa utawala huo na kusema: Matukio hayo yatawaangamiza Wazayuni.