Iran yapanda hadi nafasi ya 8 ya uzalishaji wa chuma duniani
Jumuiya ya Madini Duniani imetangaza kwamba Iran imepanda ngazi hadi nafasi ya 8 katika uzalishaji wa chuma duniani.
Jumuiya hiyo imetangaza kuwa Jumla ya uzalishaji wa chuma wa Iran duniani ulirekodi ukuaji wa asilimia 17.4 mwezi Juni 2023.
Kwa mujibu wa ripoti hii, Iran ilishika nafasi ya saba mwezi Juni na nafasi ya nane katika nusu ya kwanza ya mwaka huu (2023) katika uzalishaji wa chuma duniani.
Jumuiya ya Madini Duniani iliripoti kuwa uzalishaji wa chuma ghafi wa Iran ulifikia tani milioni 3.2 mwezi Juni mwaka huu, jambo ambalo linaonyesha ukuaji wa asilimia 17.4 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana (2022).
Nchi 63 zinazozalisha chuma kwa wingi duniani zilizalisha tani milioni 158 na laki 800 za chuma ghafi mwezi Juni mwaka huu, jambo ambalo linaonyesha kupungua kwa asilimia moja ya kumi ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Pia, katika miezi 6 ya kwanza ya mwaka huu, Iran ilizalisha jumla ya tani milioni 16 na 100 za chuma ghafi, ambayo inaonyesha ongezeko la asilimia 4.8 ikilinganishwa na kipindi kama hicho cha 2022.
Kwa kuzalisha kiasi hiki, Iran iliweza kupanda hadi nafasi ya nane katika uzalishaji wa chuma duniani katika nusu ya kwanza ya mwaka huu. Nafasi ya awali ya Iran katika uzalishaji wa chuma katika miaka ya nyuma ilikuwa ya 10.
Wakati huo huo, watengenezaji chuma duniani walizalisha tani milioni 943 na 900 elfu za chuma ghafi kuanzia mwanzoni mwa Januari hadi mwisho wa Juni 2023.
China, ikiwa na uzalishaji wa tani milioni 535 na 600 elfu, ilichangia kiwango kikubwa zaidi cha uzalishaji wa chuma ghafi duniani.