Lango la Qur'ani kujengwa jijini Tehran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i100490-lango_la_qur'ani_kujengwa_jijini_tehran
Mwenyekiti wa Baraza la Kiislamu la Jiji la Tehran amesema 'Lango la Qur'ani' litajengwa katika mji mkuu huu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 30, 2023 08:21 UTC
  • Lango la Qur'ani kujengwa jijini Tehran

Mwenyekiti wa Baraza la Kiislamu la Jiji la Tehran amesema 'Lango la Qur'ani' litajengwa katika mji mkuu huu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mehdi Chamran Mwenyekiti wa Baraza la Kiislamu la Jiji la Tehran amenukuliwa na Shirika la Habari la Iran Press akisema kuwa katika kukabiliana na kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika baadhi ya nchi za Ulaya hivi karibuni, baraza hilo litajenga lango kwa jina la Qur'ani Tukufu katika moja ya malango ya kuingilia mjini Tehran.

Ikumbukwe kuwa Siku ya Alhamisi, Julai 20, kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha wiki chache tu, raia wa Iraq na Uswidi Salwan Momika aliivunjia heshima Qur'ani Tukufu kwa msaada wa polisi ya polisi ya Uswidi; kitendo cha kishenzi ambacho kilikabiliwa na mjibizo mkubwa wa nchi za Kiislamu.

Hivi karibuni pia, wanachama wa kundi lenye misimamo ya chuki dhidi ya Uislamu la mrengo wa kulia wenye mielekeo ya kufurutu mpaka nchini Denmark liitwalo Patriots of Denmark waliuchoma moto Msahafu mbele ya ubalozi wa Iraq na wakafanya hivyo tena mbele ya balozi za Misri na Uturuki mjini Copenhagen.

Lango la Qur'ani (Darvazeh-e-Qur'an) ni lango la kihistoria latika mji wa Shiraz kusini mwa Iran na  moja ya vivutio vikuu vya kitalii katika mji huo na juu ya lango hilo kuna Misahafu miwili

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kutovukiwa adabu matukufu ya Waislamu hasa Qur'ani Tukufu huko nchini Uswidi ni tukio chungu na ni njama hatari sana akisisitiza kuwa, aliyefanya jinai hiyo lazima aadhibiwe, na maulamaa wote wa Kiislamu wanaafikiana katika hilo.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alisema hayo katika ujumbe maalumu wa maandishi na kuongeza kuwa, serikali ya Uswidi ina wajibu wa kumtia mbaroni aliyefanya jinai hiyo na kumkabidhi kwa idara za mahakama za nchi za Waislamu.