Kan'ani: Wazayuni na waungaji mkono wao wawajibishwe kwa kuwauwa watoto wa Kipalestina
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiriai takwimu zilizochapishwa kwamba watoto 37 wa Kipalestina waliuawa shahidi mwaka 2023 katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Ghaza, na kusisitiza kuwajibika wa utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake.
Nasser Kan'ani Chafi ameitaka jamii ya kimataiifa kutoa himaya na uungaji mkono haraka iwezekanvyo kwa watoto wa Kipalestina.
Katika ujumbe aliouaandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter Kan'ani amsema: Wakati maafisa wa Umoja wa Mataifa wanaonyesha wasi wasi wao wa kucheleweshwa kuanza shule za Wapalestina nchini Lebanon, kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa na Mpango wa Kulinda Watoto, utawala wa Kizayuni umeua watoto 31 katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan tangu kuanza mwaka huu (2023) na pia kuwaua watoto 6 katika Ukanda wa Gaza.
Aidha msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Iran amesema: Jumuiya na asasi za kimataifa zinapaswa kuwaunga mkono mara moja Wapalestina hususan watoto wa Kipalestina na kwanmba, Wazayuni na waungaji mkono wao wa Magharibi wanapaswa kuwajibishwa kwa jinai walizozifanya.
Ripoti mpya imeeleza kuwa, utawala huo haramu umewaua shahidi Wapalestina zaidi ya 200 tokea Januari mwaka huu hadi sasa katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Kanali ya Press TV imenukuu ripoti hiyo ikieleza kuwa, utawala huo pandikizi unawaua shahidi Wapalestina wakiwemo watoto wadogo na wanawake kila uchao mkabala wa kimya cha jamii ya kumataifa.
Aidha ripoti mpya iliyotolewa na kituo cha kutetea maslahi ya wafungwa wa Palestina cha PCPS imesema maafisa usalama wa utawala wa Kizayuni wamewatia mbaroni mamia ya watoto wa Kipalestina tokea mwanzoni mwa mwaka huu hadi sasa.