Brigedia Jenerali Heydari: Majeshi ya Iran yamesambaratisha haiba bandia ya Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i102130-brigedia_jenerali_heydari_majeshi_ya_iran_yamesambaratisha_haiba_bandia_ya_marekani
Kamanda wa Kikosi vya Nchi Kavu vya Jeshi la Iran amesema kuwa, majeshi ya Iran ya Kiislamu yamesambaratisha haiba bandia ya Marekani kutokana na kujitolea muhanga kwao na kufanya kazi kwa bidhii kubwa bila ya kuchoka.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 11, 2023 23:02 UTC
  • Brigedia Jenerali Heydari: Majeshi ya Iran yamesambaratisha haiba bandia ya Marekani

Kamanda wa Kikosi vya Nchi Kavu vya Jeshi la Iran amesema kuwa, majeshi ya Iran ya Kiislamu yamesambaratisha haiba bandia ya Marekani kutokana na kujitolea muhanga kwao na kufanya kazi kwa bidhii kubwa bila ya kuchoka.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Brigedia Jenerali Kioumars Heydari amesema hayo na kusisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo hii ina taathira kubwa katika eneo hili na duniani kiujumla.

Amesema, dunia nzima imeona jinsi Iran ilivyoipiga kwa makombora kambi kubwa ya kijeshi ya Marekani ya 'Ain al Assad ya nchini Ira na namna ilivyowafukuza Wamarekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi na namna inavyozitungua ndege zisizo na rubani za Marekani kwa ushujaa mkubwa.

Wanajeshi vamizi wa Marekani wakiwa chini ya ulinzi wa vikosi vya ulinzi vya Iran walipoingia kwenye maji ya taifa hili la Kiislamu kinyume cha sheria

 

Kamanda wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza pia kuwa, maadui wote wanapaswa kuelewa kwamba, Jamhuri ya Kiislamu imesimama imara kwenye jiografia ya muqawama na kamwe haitorudi nyuma.

Brigedia Jenerali Heydari amegusia juhudi za vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran za kuhakikisha vinajitosheleza katika kila kitu na kusisitiza kwamba, Iran leo hii haihitajii nchi yoyote ile katika upande wa kujitosheleza hasa katika uzalishaji wa zana na vifaa vya ulinzi.

Kigezo kikuu cha kiulinzi cha Iran kiasili kimesimama juu ya msingi wa kuzuia kushambuliwa kwani ni jambo la dharura mno kuwa na nguvu za kijeshi na za silaha kali na za kisasa ili kumfanya adui asifikirie kabisa kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.