Tehran na Washington kuendelea kubadilishana wafungwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i102156-tehran_na_washington_kuendelea_kubadilishana_wafungwa
Matthew Miller, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ametangaza kuwa Tehran na Washington zitaendelea na mchakato wa kubadilishana wafungwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 12, 2023 10:44 UTC
  • Tehran na Washington kuendelea kubadilishana wafungwa

Matthew Miller, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ametangaza kuwa Tehran na Washington zitaendelea na mchakato wa kubadilishana wafungwa.

Mchakato wa kuanza kuachiliwa fedha za Iran zinazoshikiliwa nje ya nchi na kubadilishana wafungwa kati ya Tehran na Washington ulitangazwa tarehe 10 Agosti baada ya miaka miwili ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amewaambia waandishi wa habari mjini Washington kwamba mchakato wa kuwaachilia huru raia wa Marekani kutoka Iran unaendelea, lakini hakutoa kutoa maelezo zaidi.

Awali, Nasser Kan'ani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alisema katika kikao cha waandishi wa habari kuhusu suala la kubadilishana wafungwa kati ya Iran na Marekani kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya pande hizo mbili kwamba: "Tuna matumaini makubwa ya kubadilishana wafungwa katika siku chache zijazo."

Nasser Kan'ani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuhusu fedha za Iran zinazozuiliwa nje ya nchi kwamba: Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa, tunatumai kuwa fedha hizo zitaletwa nchini katika siku zijazo na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itakuwa na uwezo wa kutumia mali zake.

Umekiwa umebakia zaidi ya mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa rais wa Marekani wa 2024, utawala wa chama cha Democratic wa Joe Biden, ambaye kulingana na kura za maoni, umaarufu wake unaendelea kupungua, unatafuta njia za kujinasua kutoka kwenye mikwamo ya kujitengenezea wenyewe katika uwanja wa sera za nje ili kuongeza nafasi ya kupata ushindi chama chake katika uchaguzi ujao.