Sep 17, 2023 14:00 UTC
  • Kuongezeka mabadilishano ya kibiashara kati ya Iran na Tanzania

Mkuu wa Kituo cha Biashara cha Iran na Tanzania amesema kuwa, kufanyika maonyesho ya kwanza ya kipekee ya uwezo wa usafirishaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania kuwa jukwaa linalofaa zaidi la kuongeza ufahamu wa bidhaa za Iran katika nchi za Afrika Mashariki.

Soko kubwa la Afrika ni jukwaa linalofaa kwa ajili ya kuuza bidhaa za Iran, na katika hali hiyo, Bara la Afrika lina nafasi maalum katika siasa za nje za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa msingi huo, maonyesho ya kwanza ya kipekee ya uwezo wa usafirishaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yatafanyika nchini Tanzania kuanzia Novemba 21 hadi 24 kwa idhini rasmi ya Shirika la Maendeleo ya Biashara la Iran.

Kuhusiana na hilo, Seyed Raed Mousavi, Mkuu wa Kituo cha Biashara cha Iran na Tanzania amesema katika mahojiano na Shirika la Habari IRNA kuwa: Katika maonyesho ya kwanza ya kipekee ya uwezo wa kusafirisha nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania, makampuni yanayohusiana na biashara ya mazao ya kilimo, viwanda vya kilimo na mashine, migodi na mashine za Viwanda, ujenzi, ujenzi, dawa na vifaa tiba zitashiriki, jambo ambalo ishara njema za kuimarishwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika fremu ya ushirikiano wa kiuchumi.

Marais wa Iran na Tanzania walipofanya mazungumzo pambizoni mwa mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini

 

Mousavi amebainisha kwamba, kuwepo kwa makampuni ya Iran na wafanyabiashara wa Tanzania katika maonyesho hayo na kuandaliwa mazungumzo ya kibiashara kati ya sekta binafsi na ya umma ya Iran na Tanzania ndio kipaumbele cha kituo hiki na hilo litaendelezwa.

Mkuu wa kituo cha kibiashara cha Iran nchini Tanzania amesema: Kwa kuzingatia njia ya moja kwa moja ya usafirishaji wa meli na mizigo na urahisi wa kupeleka bidhaa Tanzania, tunajaribu kuandaa mazingira yanayofaa kwa ajili ya mazunguumzo katika mstari wa kibiashara na pia kuweza kupanua biashara kwa kuhudumia soko la Afrika Mashariki.

Tags