Abdollahian: Kuzingatia mhimili wa muqawama ni sera za kimsingi za nchi yetu
Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri yaa Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuzingatia mhimili wa muqawama ni sera za kimsingi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Adollahiana maesema hayo hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na gazeti la al-Wifaq na kusisitiza uungaji mkono wa kudumu wa Iran kwa ajili ya uthabiti na usalama katika eneo na katika kuwalinda wanaodhulumiwa na wanyonge.
Amir Abdollahian amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeweka katika ajenda yake suala la kushirikiana na kuwa na maingiliano na Mashariki na Magharibi ya dunia kwa lengo la kupata maslahi ya kitaifa na kwa minajili ya kupata uhuru wake wa kisiasa, na muqawama unahesabiwa kuwa moja ya mielekeo muhimu katika sera za kigeni za Jamhuri ya Kiislamu.
Akiashiria matukio ya Syria, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, ulimwengu wa Kiarabu wenye mtazamo mpya nchini Syria unashughulika na kufungua milango, kuirejesha Syria kwenye Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, kufungua tena balozi na kuanzisha ushirikiano katika ngazi tofauti na nchi hiyo ya Kiarabu.
Akigusia matukio ya Ukraine, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran pia alisema kuwa, Tehran haijatoa ndege zozote zisizo na rubani kwa Warusi kuzitumia katika vita hivyo, bali kuhusu suala la muqawama wa Palestina na Lebanon licha ya madhara iliyonayo misimamo hiyo, lakini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza bayana kwamba Iran iko pamoja na muqawama.