Meja Jenerali Baqeri: Mhimili wa muqawama hauihitaji tena Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i102374-meja_jenerali_baqeri_mhimili_wa_muqawama_hauihitaji_tena_iran
Mkuu wa Komandi Kuu ya Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria uwezo wa mhimili wa muqawama katika kuunda silaha na kusema hii leo mhimili huo umejitosheleza na hauhitajii Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 18, 2023 04:43 UTC
  • Meja Jenerali Baqeri
    Meja Jenerali Baqeri

Mkuu wa Komandi Kuu ya Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria uwezo wa mhimili wa muqawama katika kuunda silaha na kusema hii leo mhimili huo umejitosheleza na hauhitajii Iran.

Meja Jenerali Muhammad Baqeri amesema kuwa kuasisiwa mhimili wa muqawama ni moja ya mafanikio ya kujihami kutakatifu na kwamba mhimili wa muqawama hauihitajii tena Iran kwa sababu wenyewe unaunda silaha kujitegemea pakubwa. 

Meja Jenerali Baqeri ameendelea kubainisha kuwa, kaulimbiu ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya 'Kuanzia Nile hadi Furati' haijasahaulika na kuongeza kuwa, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu limepanua na kuimarisha misingi ya Hizbullah na makundi ya mapambano huko Palestina; na hii leo utawala wa Kizayuni umefika mahali ambapo viongozi wake wanasema kuwa, kupanuka kwa muqawama wa Palestina kumewasababishia matatizo makubwa. 

Wanamuqawama wa Palestina 

Mkuu wa Komandi Kuu ya Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria pia vikwazo vya Magharibi dhidi ya wananchi wa Iran na kusema, Iran iliwahi kuwekewa vikwazo vya kutonunua chochote, lakini leo hii imezuiwa kutouza chochote.  

Meja Jenerali Baqeri amesema hii leo wateja wa ndege zisizo na rubani za Iran (droni) wameongezeka zaidi ya uwezo wa uzalishaji wa nchi, huku nchi kubwa duniani zikitaka kununua silaha za Iran.