Sep 26, 2023 07:57 UTC
  • Eslami akosoa mienendo ya nchi za Magharibi kuhusu Iran

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amekosoa mienendo ya nchi za Magharibi na kusema: nchi hizo hutumia uwezo wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kuishinikiza Iran.

Mohammad Eslami Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki (AEOI) amekutana na Rafael Grossi Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) pambizoni mwa Kikao cha 67 cha Kawaida cha Baraza Kuu la Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) mjini Vienna siku ya Jumatatu;ambapo wawili hao walikuwa na mazungumzo kuhusu kustawisha ushirikiano wa kiufundi kati ya Iran na Wakala wa IAEA na kustawisha uhusiano wa pande mbili.  

Eslami na Grossi pia walijadili na kubadilishana mawazo kuhusu njia mbalimbali za kustawisha ushirikiano wa pande mbili. 

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa pia mienendo ya nchi za Magharibi na akasema: Nchi hizi zinajaribu kutumia uwezo wa IAEA kuishinikiza Iran kupitia mashinikizo ya kisiasa na kuiwekea vikwazo.  

Mohammad Eslami pia amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kudumisha mismamo wa kutoegemea upande wowote na kuzingatia weledi katka utendaji wake na kutoruhusu nchi hizo kutumia ripoti za wakala huo kama kisingizio cha kuishinikiza Iran.

Muhammad Eslami