Iran na Saudia zahimiza ushirikiano wa kielimu, kiteknolojia na kiutafiti baina yao
Naibu Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia wa Iran, na Mkuu wa Mji wa Elimu na Teknoljia wa Saudi Arabia wametangaza utayari wa nchi zao wa kushirikiana kielimu, kiteknolojia na kiutafiti kupitiaa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC.
Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Naibu Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia wa Iran, Peyman Salehi, ameonana na Mkuu wa Mji wa Elimu na Teknoljia wa Saudia, Munir bin Mahmoud El-Desouki, pambizoni mwa kikao cha STS mjini Kyoto Japan na sambamba na pande hizo mbili kutilia mkazo wajibu wa kushirikiana zaidi nchi za Kisilamu zimehimiza kuweko ushirikiano mkubwa zaidi wa kielimu, kiteknolojia na kiutafiti baina ya pande mbili na pande kadhaa ndani ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislalmu OIC.
Katika mazungumzo hayo, nchi mbili za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia zimeainisha pia nyuga zenye manufaa ya pamoja na zilizo muhimu zaidi katika kuongeza ushirikiano wa kielimu na kiteknlojia baina yao na kuhimiza kuwa, kadiri nchi za Kiislamu zitakavyokuwa na ushirikiano zaidi katika masuala ya kielimu ndivyo Ulimwengu wa Kiislamu utakavyoweza kunufaika zaidi na fursa zilizopo kama ambavyo pia hiyo ni fursa nzuri ya kuimarisha zaidi na zaidi ushirikiano wa nchi hizi mbili katika masuala mengineyo siku za usoni.
Katika muundo mpya wa uongozi wa serikali ya Saudia, Mkuu wa Mji wa Elimu na Teknoljia wa nchi hiyo ni mtu mwenye cheo kikubwa zaidi cha masuala ya utafiti na teknolojia na ana jukukmu la kusaidia miradi yote ya ubunifu na utafiti ya Saudi Arabia.