Mazungumzo ya Rais wa Iran na viongozi wa Hamas na Jihadul-Islami
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul Islami na Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas).
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iranpress, katika mazungumzo hayo Seyyed Ebrahim Raisi amezungumzia kwa nyakati tofauti kuhusu matukio ya Palestina na Ziad Al-Nakhleh, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul Islami na Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina. Hamas.
Mazungumzo hayo yamefanyikka kkatika hali ambayo, Jana tarehe 7 Oktoba 2023 Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas ilitekeleza oparesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa dhidi ya utawala ghasibu wa Israel, jambo ambalo limeshtua na kuuwacha utawala huo kinywa wazi.
Vikosi vya Brigedi ya Qassam, tawi la kijeshi la Hamas, vimefanya mashambulizi makubwa ya roketi na ya nchi kavu dhidi ya Israel.
Operesheni hiyo kubwa na tata ya Muqawama wa Palestina, ambayo ilifanyika kwa kutumia njia za chini ya ardhi, nchi kavu, baharini na angani, pamoja na kurusha maelfu ya maroketi na makombora katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, hadi sasa imepelekea kuangamizwa Mamia ya Wazayuni na kujeruhiwa wengine zaidi ya 1,600.
Mashambulio makubwa na ya kushtukiza ya nchi kavu, anga na baharini ya wanamapambano wa Kipalestina dhidi ya walowezi wa Kizayuni wanaokaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina, yaliyopewa jina la Kimbunga cha Al-Aqsa yamepata uungaji mkono mkubwa wa kieneo na kimataifa.