Kan'ani: Hivi haki za binadamu zinajumuisha pia Palestina?
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i103558-kan'ani_hivi_haki_za_binadamu_zinajumuisha_pia_palestina
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameihutubu jamii ya kimataifa na kuiuliza, hivi haki za binadamu zinajumuisha pia Palestina?
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 16, 2023 10:11 UTC
  • Kan'ani: Hivi haki za binadamu zinajumuisha pia Palestina?

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameihutubu jamii ya kimataifa na kuiuliza, hivi haki za binadamu zinajumuisha pia Palestina?

Nasser Kan'ani Chafi amesema, wale wanaodai kutetea haki za binadamu na ambao wanatekeleza malengo yao ya kisiasa kwa kutumia mashinikizo hii leo wameifumbia macho kabisa Gaza na dhulma inayofanywa dhidi ya wananchi wa Palestina.

Nasser Kanani, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema hayo katika mkutano wake wa kila wiki na waandishi wa habari na kkuueleza kwamba, katika siku za hivi karibuni, tumeshuhudia muqawama wa wananchi majasiri ambao wana historia ya kuwepo miaka 1000 huko Palestina na Gaza na katika masikkuu haya, historia ya zaidi ya miaka 70 ya jinai za Wazayuni inajirudia.

Kuhusiana na matukio ya hivi karibuni ya Gaza, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema: Kilichofanyika ni hatua ya harakati za Palestina kujibu hatua za utawala wa Kizayuni, na madai ya kutumwa majeshi ya Iran ni ya uongo mtupu.

 

Akionyesha picha zenye kuakisi uchungu za Gaza, Kan'ani amesema kkwa kuhoji, hivi haki za binadamu zinajumuuisha pia Palestina?

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ammesisitiza kuwa: Serikali ya Marekani inapaswa kuwajibishwa kwa jinai za utawala wa Kizayuni; kutia nanga meli ya kijeshi kwenye maji ya eneo hakuna maana yoyote isipokuwa kumuunga mkono dhalimu mbele yya mdhulumiwa, na yeyote atakayeuunga mkono utawala wa Kizayuni anabeba dhima na jukumu la kimataifa.