Kan'ani: Kushtakiwa watenda jinai wa Kizayuni ni takwa la wapigania uadilifu duniani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i103758-kan'ani_kushtakiwa_watenda_jinai_wa_kizayuni_ni_takwa_la_wapigania_uadilifu_duniani
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza na kusema kuwa, kushtakiwa watenda jinai wa Kizayuni ni takwa la wapigania uadilifu kote duniani.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Oct 21, 2023 09:36 UTC
  • Kan'ani: Kushtakiwa watenda jinai wa Kizayuni ni takwa la wapigania uadilifu duniani

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza na kusema kuwa, kushtakiwa watenda jinai wa Kizayuni ni takwa la wapigania uadilifu kote duniani.

Nassir Kan'ani Chafi ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii: Baada ya maafa ya Hospitali ya al-Ma'madani, kubomoa baadhi ya misikiti, kanisa na shule, kwa mara nyingine tena utawala huo ghasibu umetoa vitisho vya kushambulia hospitali zingine katika Ukanda wa Gaza.

Kanani ameongeza kuwa, jinai hizo za kutisha zina maana kwamba, utawala wa Kizayuni umevuka mpaka wa wendawazimu na ni kashfa kubwa na ya aibu ya kimaadili kwa tawala ambazo zimeendelea kuukingia kifua na kuuunga mkono utawala huo katili bila ya masharti yoyote na wakati huo huo zinahubiria mataifa mengine na kutaka kuyafundisha haki za binadamu.

 

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kuwa, uvamizi, hujuma, vita, uhalifu, ugaidi, mauaji ya halaiki, mauaji ya watoto, mashambulizi dhidi ya misikiti, makanisa, hospitali, magari ya kubebea wagonjwa na magari ya misaada, shule, nyumba na makazi, kambi za wakimbizi, waandishi wa habari n.k., ni uhalifu unaofanywa hii leo ulimwenguni na utawala ghasibu wa Israel uhalifu ambao umedumu kwa miaka zaidi ya 70.

Kadhalika Kan'ani amesisitiza kuwa, hii leo kutangazwa na kutambuliwa kimataifa utawala wa Kizayuni kuwa ni utambulisho wa kigaidi na kuwafungulia mashtaka na kuwahukumu wahalifu wa kivita wa Kizayuni ni takwa la watu wote walio huru, wenye kutetea na kupigania na uadilifu duniani.