Kuna wajibu wa kupandishwa kizimbani waungaji mkono wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i105214-kuna_wajibu_wa_kupandishwa_kizimbani_waungaji_mkono_wa_israel
Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa ya Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu (Bunge la Iran) amelaani kimya cha baadhi ya viongozi wa nchi za dunia mbele ya jinai za utawala wa Kizayuni na kusisitiza kuwa, kuna wajibu wa kupandishwa kizimbani waungaji mkono wa Israel kwa kushiriki kwenye jinai za utawala huo dhalimu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 25, 2023 03:31 UTC
  • Kuna wajibu wa kupandishwa kizimbani waungaji mkono wa Israel

Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa ya Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu (Bunge la Iran) amelaani kimya cha baadhi ya viongozi wa nchi za dunia mbele ya jinai za utawala wa Kizayuni na kusisitiza kuwa, kuna wajibu wa kupandishwa kizimbani waungaji mkono wa Israel kwa kushiriki kwenye jinai za utawala huo dhalimu.

Hadi hivi sasa karibu Wapalestina 15,000 wameshauwa shahidi na zaidi ya 36,000 wengine wameshajeruhiwa kwenye mashambulizi ya kijinai na kikatili ya utawala wa Kizayuni huko Ghaza. Asilimia kubwa ya wahanga wa ukatili huo ni wanawake na watoto wadogo.

Shirika la habari la IRNA limemnukuu Vahid Jalalzadeh, Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni ya Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu (Bunge la Iran) akisema kuwa, utawala wa Kizayuni umefanya jinai kubwa ya kuua shahidi wanandhi wasio na hatia wa Palestina, wanaume, wanawake na watoto wachanga kiasi kwamba zaidi ya raia 14,000 wa Palestina wameshauawa shahidi huku baadhi ya viongozi na taasisi za barani Ulaya zinazodai kupigania haki za binadamu likiwemo Bunge la Ulaya, zikiendelea kunyamazia kimya jinai hizo za kuchupa mipaka. 

Jalalzadeh amegusia jinsi baadhi ya wabunge wa Ulaya walivyojitokeza hadharani kuunga mkono jinai za Wazayuni na kusema kuwa, ni jambo lisilo na chembe ya shaka kwamba baadhi ya viongozi wa nchi za Ulaya wanahusika na jinai za Israel dhidi ya watu wasio na hatia huko Ghaza na kwamba kama ilivyo wajibu wa kupandishwa kizimbani viongozi watenda jinai za Israel, ni vivyo hivyo, kuna udharura wa kuburuzwa mahakamani waungaji mkono wao.