Rais Raisi: Uingiliaji wowote wa Marekani katika masuala ya Gaza utashindwa tu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i105288-rais_raisi_uingiliaji_wowote_wa_marekani_katika_masuala_ya_gaza_utashindwa_tu
Seyed Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amesema watu wa Gaza, kupitia Hamas ambayo ni serikali halali na ya kisheria iliyochaguliwa kwa kura za wananchi wa eneo hilo, ndio wanaopasa kuamua juu ya mustakbali wa Gaza; na Marekani haina haki ya kuingilia kwa namna yoyote na kufanya maamuzi kwa ajili ya watu wa Gaza; na hatua yoyote itakayochukua juuu ya suala hilo itashindwa tu.
(last modified 2026-05-19T09:45:50+00:00 )
Nov 27, 2023 00:00 UTC
  • Rais Raisi: Uingiliaji wowote wa Marekani katika masuala ya Gaza utashindwa tu

Seyed Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amesema watu wa Gaza, kupitia Hamas ambayo ni serikali halali na ya kisheria iliyochaguliwa kwa kura za wananchi wa eneo hilo, ndio wanaopasa kuamua juu ya mustakbali wa Gaza; na Marekani haina haki ya kuingilia kwa namna yoyote na kufanya maamuzi kwa ajili ya watu wa Gaza; na hatua yoyote itakayochukua juuu ya suala hilo itashindwa tu.

Kwa mujibu wa IRNA, katika mazungumzo aliyofanya kwa njia ya simu na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki Jumapili usiku, Seyed Ebrahim Raisi ameuelezea uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuwa wa kirafiki, wa kihistoria na unaozingatia ujirani mwema, maadili ya kidini na maslahi ya pamoja ya mataifa hayo mawili, na akasema, kuimarisha na kuinua kiwango cha ushirikiano na mahusiano ya Tehran na Ankara kuna umuhimu katika nyanja tofauti za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.
 
Raisi amezitaja Iran na Uturuki kuwa nchi mbili muhimu na zenye taathira katika Ulimwengu wa Kiislamu na akaeleza matumaini yake kuwa ushirikiano wa pamoja kati ya nchi hizi utakuwa kigezo cha maelewano kati ya nchi za Kiislamu.
 
Katika sehemu nyingine ya mazungumzo hayo Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Marekani ndiyo muuaji wa watu wa Gaza na akasisitiza kwamba uingiliaji wowote wa Marekani katika mustakbali wa Gaza ni mwendelezo wa jinai za nchi hiyo dhidi ya haki za Wapalestina.
Mkuu wa Hamas, Ismail Haniya (kushoto) na Yahya Sinwari, Mkuu wa harakati hiyo Gaza

Seyed Ebrahim Raisi ameashiria namna Marekani ilivyotoa ushirikiano na kusimamia uhalifu wa kutisha wa utawala wa Kizayuni na mauaji ya halaiki uliyofanya utawala huo dhidi ya watu madhulumu wa Gaza, na akabainisha pia jinsi serikali ya Marekani ilivyofedheheka na kupoteza heshima mbele ya wananchi wa mataifa na akasema: watu wa Gaza, kupitia Hamas ambayo ni serikali halali na ya kisheria iliyochaguliwa kwa kura za wananchi wa eneo hilo, ndio wanaopasa kuamua juu ya mustakbali wa Gaza; na Marekani haina haki ya kuingilia kwa namna yoyote na kufanya maamuzi kwa ajili ya watu wa Gaza; na hatua yoyote itakayochukua juuu ya suala hilo itashindwa tu.

 
Kwa upande wake, Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki yeye ameashiria uhusiano mzuri na wenye kujenga uliopo kati ya Tehran na Ankara na akasisitiza juu ya kufanywa juhudi za kuinua uhusiano huo kwa kiwango cha juu zaidi na cha kipekee.
 
Erdoğan amebainisha pia utayari wa nchi yake kuitisha mkutano wa Baraza Kuu la Ushirikiano kati ya nchi mbili.../