Kan'ani: Utawala wa Kizayuni ni hatari kwa dunia nzima na ubinadamu
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, utawala wa Kizayuni ni utawala wa ubaguzi wa rangi na ni tishio kwa ubinadamu na dunia nzima.
Shirika la habari la Tasnim limemnukuu Nasser Kan'ani akisema hayo kwenye mtandao wa kijamii wa X sambamba na kusambaza picha za wananchi wa Palestina waliotekwa nyara na kuvuliwa nguo na wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran vile vile amesema, jinai ya utawala wa Kizayuni ya kuwateka nyara na kuwavua nguo raia wa Palestina na baadaye kuwapiga picha na kuzisambaza kote ulimwenguni, mwito wa naibu meya Mzayuni wa mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na Wazayuni, wa kuwataka viongozi wa Tel Aviv kuwazika hai mateka wa Palestina, hatua ya waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni wa kuwaita Wapalestina kuwa ni wanyama wenye sura za watu, na mwito wa waziri wa turathi ya wa utawala wa Kizayuni wa kuitaka Israel iishambulie Ghaza kwa bomu la nyuklia, ni mambo ambayo kivitendo yanaonesha sura isiyo na chembe ya ubinadamu ya utawala wa Kizayuni na jinsi utawala huo mbaguzi wa rangi ulivyo hatari sana kwa wanadamu wote duniani.
Kabla ya hapo, Kituo cha wakimbizi wa Palestina kilikuwa kiimetangaza kwamba jeshi katili la utawala dhalimu wa Israel linawanajisi kikatili mateka wa Kipalestina hasa wanawake na watoto wadogo.
Mashirika ya haki za binadamu yametoa ushahidi mwingi wa jinsi wanajeshi na maafisa wa utawala wa Kizayuni wanavyowanajisi na kuwadhalilisha kijinsia mateka wa Kipalestina ambao kama wanavyosema waziwazi na bila kisisi viongozi wa utawala katili wa Israel, kwamba kwa mtazamo wao Wapalestina si binadamu, ni wanyama wenye sura za watu na mashirika hayo yamelaani vikali jinai hizo za Wazayuni.