Bagheri Kani: Uhusiano wa Iran na Saudi Arabia uko kwenye mkondo sahihi
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika Masuala ya Kisiasa amesema kuwa, uhusiano kati ya Iran na Saudi Arabia uko kwenye mkondo sahihi.
Ali Bagheri Kani amesema kuwa, katika fremu ya makubaliano ya Beijing kati ya viongozi watatu wa ngazi za juu wa Iran, China na Saudi Arabia, kamati ya pamoja ya pande tatu itaundwa kila baada ya miezi sita ili kupitia upya matarajio ya uhusiano wa pande mbili na wa pande kadhaa.
Bagheri Kani amesema kuhusiana na matokeo ya mkutano wa pande tatu kati ya Iran, China na Saudi Arabia mjini Beijing kwamba, "mkutano huo ulikuwa mzuri sana na wenye kujenga na mambo yenye manufaa yalijadiliwa katika mkutano wa Beijing."
Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iran pia katika kujibu swali la mwandishi wa habari wa Iran Press huko Beijing kuhusu hali ya uhusiano wa Tehran na Riyadh, amesisitiza kwamba uhusiano wa Iran na Saudia umeingia katika mwelekeo na mkondo sahihi na nchi hizo mbili zinafanya kazi kwa nia ya dhati kwa minajili ya kuboresha uhusiano wao.
Bagheri Kani amesisitiza kuwa, Iran na Saudi Arabia zina uwezo mzuri wa kupanua na kukuza uhusiano wa pande mbili, na jambo muhimu ni kwamba uhusiano huo hautaishia kwenye uhusiano wa Tehran na Riyadh pekee, bali matokeo chanya ya uhusiano wa pande mbili yatakuwa na taathira chanya kieneo na maendeleo ya dunia.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa alisema, "Iran na Saudi Arabia ni nchi mbili kubwa zenye akiba ya nishati, na kwa maana hii, zina nafasi maalumu duniani ya kuzitegemea.