Dec 18, 2023 07:20 UTC
  • Kuundwa miundombinu ya pamoja kati ya Irani na Russia kwa ajili ya kuimarisha mashirika yenye msingi wa maarifa

Mkuu wa Shirika la Maendeleo na Biashara la Iran ametilia mkazo juu ya kuundwa miundombinu ya pamoja kati ya Iran na Russia kwa ajili ya kuboresha mashirika ya msingi wa maarifa.

Katika miaka ya hivi karibuni, na licha ya vikwazo, makampuni yanayojikita katika msingi wa maarifa ya Iran yameweza kujipatia nafasi muhimu katika masoko ya kimataifa kutokana na ujuzi wao na uwezo wa juu wa kisayansi na uzalishaji.

Mehdi Zaighami, Mkuu wa Shirika la Maendeleo na Biashara amesema katika mahojiano na shirika la habari la IRIB kwamba Iran na Russia zina uwezo mkubwa katika mfumo wa misingi ya maarifa hivyo zinaweza kukidhi mahitaji ya kila upande na vilevile kutoa huduma nzuri kwa eneo la Eurasia.

Mkuu huyo wa Shirika la Maendeleo na Biashara ameongeza kuwa miundombinu inayotegemea msingi wa maarifa katika eneo la Eurasia imejadiliwa na pande mbili.

Akizungumzia kuanzishwa maeneo ya biashara huria ya pamoja, mkuu wa Shirika la Maendeleo na Biashara amesema: Tunachunguza na baadhi ya nchi kama vile Russia uwezekano wa kuanzishwa eneo  la pamoja la biashara.

 

Tags