Kan'ani: Msingi wa Israel umejengwa kwa kutegemea mabavu na ubaguzi
(last modified Sat, 27 Jan 2024 12:25:39 GMT )
Jan 27, 2024 12:25 UTC
  • Nasser Kan\\\'ani
    Nasser Kan\\\'ani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa jibu la kiuhasama lililotolewa na utawala wa Kizayuni wa Israel mkabala wa hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) linaonyesha namna msingi wa utawala huo ulivyojengwa kwa kutegemea vitendo vya mabavu na ubaguzi; na wakati huo huo unadhihirisha namna utawala huo usivyoheshimu kanuni na sheria za kimataifa.

Mahakama ya ICJ jana ilitoa hukumu kuhusu kesi iliyofunguliwa na  Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu jinai za mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo Ukanda wa Gaza na ulazima wa kuchukuliwa hatua za dharura katika eneo hilo la Palestina. 

Hukumu hiyo inaeleza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unapasa kuchukua hatua za lazima kuzuia jinai za mauaji dhidi ya binadamu huko Gaza. Utawala huo unapasa kuhakikisha kuwa wanajeshi wake hawatekelezi mauaji ya kimbari na kuchukua hatua za kuboresha hali ya kibinadamu huko Gaza. 

Kwa msingi huo, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema katika radiamali yake kwa hukumu hiyo ya ICJ wamba: Tuhuma za mauaji ya kimbari ni kali na za kushtua na kwamba vita vitaendelea huko Gaza.  

Nasser Kan'ani Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran mapema leo Jumamosi ameandika katika  ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kuhusu hukumu ya mahakama ya ICJ dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ukanda wa Gaza kwamba: Ijapokuwa hukumu hii imechelewa, lakini ni uthibitisho wa ukweli mchungu kwamba yanayotokea Gaza ni mfano wa wazi wa jinai za kimataifa yakiwemo mauaji ya kimbari ambayo yametekelezwa na yanaendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni kwa uungaji mkono wa pande zote wa serikali ya Marekani. 

Tags