Iran yatuma angani salalaiti ya utafiti ya Pars-1 iliyotengenezwa nchini
(last modified Fri, 01 Mar 2024 03:01:30 GMT )
Mar 01, 2024 03:01 UTC
  • Iran yatuma angani salalaiti ya utafiti ya Pars-1 iliyotengenezwa nchini

Iran jana Alhamisi ilifanikiwa kurusha angani salalaiti yake ya utafiti iliyotengenezwa na wataalamu wa hapa nchini.

Satalaiti hiyo ya Pars-1 yenye uzito wa kilo 134  ilirushwa angani jana Alhamisi na roketi la Soyuz kutoka eneo la Vostochny Cosmodrome katika jimbo la Amur nchini Russia. Huku ikiwa na  kamera tatu, satalaiti ya Pars -1 itachanganua miundo na maumbo katika ardhi ya Iran kutoka kwenye obiti umbali wa kilomita 500 juu ya uso wa Dunia.

Satalaiti hii tajwa Setilaiti imeundwa na  wataalamu na wanasayansi wachanga katika Taasisi ya Utafiti wa Anga ya Iran kwa ushirikiano wa makampuni yanayotegemea maarifa.

Akizungumza kwa njia ya televisheni, Issa Zarepour Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Iran ameeleza kuwa satalaiti hiyo itajumuishwa na satalaiti nyingine za Iran; na kwamba picha na data zake zilizotumwa zitatumika kwa shughuli mbalimbali.

Issa Zarepour 

Zarepour ameongeza kuwa Iran imerusha angani satalaiti 12 katika kipindi cha miezi 25 iliyopita. Amesema, sekta ya anga ya nchi hii inapiga hatua kwa kasi. Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Iran amesema Iran inajenga kituo kikubwa zaidi cha kurushia satalaiti katika eneo la Asia Magharibi. Kituo hicho kinajengwa kusini mwa Iran.

 

Tags