Rais Raisi: Iran ya leo imeendelea na ni ya teknolojia
Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran ya Kiislamu ya leo imeendelea na ni ya teknolojia.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kiwanda cha Zamzam 3 cha Kampuni ya Feleji ya Khuzestan kimejengwa na kuzinduliwa kwa kushirikisha makampuni 115 ya ubunifu wa utaalamu na makampuni zaidi ya 50 ya viwanda vya ndani bila kujumuisha wataalamu wa kigeni na akaongeza kuwa, tani milioni mbili za chuma cha sponji zinazalishwa nchini Iran; na katika uwanja huo, Iran ya Kiislamu inashika nafasi ya kwanza katika eneo hili na ya pili duniani; na hiyo ni heshima kubwa.
Akizungumzia kuanza kazi rasmi visima vya mafuta vya Jafir na Sepehr vilivyoko magharibi mwa Karon, Rais Raisi amesema: maeneo hayo ya mafuta yameanzishwa kwa ushirikishaji na uwekezaji wa benki za Iran, na huo ndio uwekezaji bora zaidi unaopasa kuongezwa kadiri iwezekanavyo.../