Apr 13, 2024 02:11 UTC
  • Kuendelea kuimarika uhusiano wa kiuchumi wa Iran na nchi za Kiislamu

Mkuu wa Forodha wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa, biashara kati ya Iran na nchi 56 wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) mwaka 1402 Hijria Shamsiya iliongezeka kwa asilimia 19 na kufikia dola bilioni 61.

Muhammad Rizvanfar ameongeza kuwa, bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 29 ziliuzwa nje ys ncchi, na dola bilioni 32 zimetumiwa kuagiza bidhaa kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu mwaka 1402 Hijria Shamsiya.  

Mwaka jana, Iran iliuza bidhaa zake nyingi kwa nchi wanachama wa OIC yaani Iraq, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Uturuki, Pakistan, Afghanistan, Oman, Indonesia na Jamhuri ya Azerbaijan.  

Katika kipindi hicho, mauzo ya nje ya Iran  huko Cameroon, Gambia, Misri, Brunei na Yemen yaliongezeka zaidi

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ni taasisi ya pili kubwa zaidi duniani baada ya Umoja wa Mataifa na ina nchi wanachama 57 katika mabara manne ya dunia.  Idadi ya Waislamu duniani ni zaidi ya watu bilioni mbili, ambao ni zaidi ya asilimia 25 ya watu wote duniani. 

Suala la ushirikiano baina ya nchi za Kiislamu ili kuboresha uhusian ni takwa muhimu la nchi wanachama. Tukitupia  jicho hali ya kiuchumi ya nchi wanachama wa OIC, tunaweza kushuhudia vyema kwamba nchi 57 wanachama zina uwezo mkubwa wa kuboresha na kupandisha juu nafasi na hadhi yao kimataifa. Kwa mfano, katika sekta ya uzalishaji wa kimataifa wa mafuta, ambayo ni nishati kuu ya vituo vya kiuchumi duniani, zaidi ya asilimia sabini ya mafuta huzalishwa katika nchi wanachama au waangalizi wa jumuiya ya OIC. 

Nchi wanachama wa OIC 

Katika miaka iliyopita, waratibu mipango ndani ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu wamejaribu kupanua biashara kati ya nchi za Kiislamu kwa kutumia njia mbalimbali.  Kwa kuwa nchi nyingi za Kiislamu zina mfungamano na muungano wa kijiografia kuanzia Morocco huko kaskazini mwa bara la Afrika hadi Indonesia, kusini mashariki mwa Asia zimeandaliwa nafasi na mazingira maalumu kwa upande wa kijiopolitiki inayoziwezesha kubadilishana na kusafirisha bidhaa kwa urahisi, kurahisisha utendaji kazi, wafanyakazi na vifaa vya dharura vya uzalishaji kwa ajili ya nchi hizo.  

Hatua hii- iwapo itaambatana na kufutwa kwa viza kati ya nchi za Kiislamu, pamoja na kuondolewa au kupunguzwa tozo la ushuru wa forodha- itapelekea kushuhudiwa mabadiliko ya msingi katika uhusiano kati ya nchi wanachama.

Mapendezo mengi yametolewa kuhusu kutumia uwezo wa ndani ya jumuiya ya OIC ikiwa ni pamoja na kuanzisha soko la nchi za Kiislamu kwa kuzingatia chapa ya Halal. Chapa ya Halal inazijumuisha nchi zote za Kiislamu; na uwezo huu wa OIC unaweza kutumika kwa njia bora ili kuendeleza mahusiano ya kibiashara na kiuchumi kati ya nchi za Kiislamu. 

Wakati huo huo, chombo cha sera za kigeni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kinafuatilia kwa makini hali ya mpito ya mfumo wa kimataifa kutoka mfumo wa kambi moja hadi mfumo wa kambi kadhaa; na hivyo kutambua udharura wa kuwepo maelewano na ushirikiano zaidi bana ya nchi za Kiislamu, kurejesha amani na usalama wa kiadilifu na kuratibu mipango mipya. 

Iran pia inaamini kuwa, kuwepo umoja na mshikamano kati ya nchi za Kiislamu kutazidisha uwezo na ushawishi wa Ulimwengu wa Kiislamu kulingana na rasilimali zake kubwa za kiroho na kimaada khususan uwezo wa nchi za Kiislamu wa kuimarisha ustaarabu na utamaduni wa dini ya Kiislamu. 

Katika upande mwingine kushirikiana na kuwa na umoja nchi za Kiislamu katika masuala ya pamoja ya kihistoria na kidini ni hazina na mtaji mkubwa, na kushirikiana kwa mujibu wa misingi hiyo kutaimarisha urafiki, nia njema, kudhamini ustawi wa kiuchumi kati ya nchi za Kiislamu na kurejesha amani na utulivu kati ya nchi hizo. 

Mtazamo wa Serikali ya Awamu ya 13 ya Iran wa kufuata sera ya ujirani mwema huku Iran ikiimarisha uhusiano na nchi jirani ambazo nyingi ni nchi za Kiislamu, unaweza kutathminiwa katika uwanja huo. 

Serikali ya Awamu ya 13 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran 

 

Tags