Imethibitishwa: Rais Ebrahim Raisi na wenzake wameaga dunia katika ajali ya helikopta
(last modified Mon, 20 May 2024 04:50:52 GMT )
May 20, 2024 04:50 UTC
  • Imethibitishwa: Rais Ebrahim Raisi na wenzake wameaga dunia katika ajali ya helikopta

Habari iliyotufikia hivi punde inasema kuwa, imethibitika kuwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Ebrahim Raisi ameaga dunia akiwa na wenzake kadhaa katika ajali ya helikopta iliyotokea jana katika mkoa wa Azarbaijan Kashariki, kaskazini magharibi mwa Iran.

Televisheni ya taifa ya Iran imetangaza kuwa, imethibitishwa kuwa Rais Ebrahim Rais ameaga dunia katika ajali hiyo, na tayari baraza la mawaziri linakutana kupanga taratibu za kuaga mwili wa Rais na wazaidizi wake, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir Abdollahian aliyekuwa pamoja na Rais katika ajali hiyo.

Helikopta hiyo ilikuwa imembeba Raisi Ebrahim Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian, Gavana wa mkoa wa Azarbaijan Mashariki Malek Rahmati, Imam wa Swala ya Ijumaa na mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu huko Tabriz, Mohammad Ali Al- Hashem na maafisa wengine kadhaa wa serikali.

 

 

 

Tags