Sep 07, 2024 03:12 UTC
  • Iran: Adui anatiwa kiwewe na ustawi na maendeleo yetu ya nyuklia

Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran amezungumzia maendeleo ya kupigiwa mfano iliyopata Jamhuri ya Kiislamu katika upande wa nishati ya nyuklia na kusema kuwa, licha ya kuweko vikwazo haramu vya Marekani dhidi yetu, lakini tumepiga hatua kubwa za maendeleo; na mabeberu wanatiwa kiwewe na ustawi wetu wa nyuklia.

Mohammad Eslami pia amesema, maneno yanayotolewa na mabeberu na Wazayuni hayatokani na hofu ya bomu la nyuklia bali hofu yao ni nguvu za kimaendeleo za Iran katika matumizi ya amani ya nishati ya atomiki.

Amesema, wanasayansi na wataalamu wa Iran wamepiga hatua kubwa ambazo zimewatia hofu maadui kuhusu nguvu za kiviwanda na kiuchumi za Iran.

Mkuu huyo wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran vile vile amesema kuwa, ustawi wetu wa nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani unaleta taathira nzuri za moja kwa moja katika maisha ya wananchi wetu.

Vile vile amegusia vita vya kiuchumi vinavyoendeshwa na maadui dhidi ya Iran kwa shabaha ya kuangusha thamani ya sarafu ya taifa ya Iran na kusisisitiza kuwa, istiqama na kusimama kidete wananchi wa Iran kumepelekea kuchorwa mpaka baina ya haki na batili, siasa zote za mabeberu ni kutoa vitisho na kuunga mkono uvamizi na ndio maana siasa kuu za madola ya kiistikbari ni kutumia vikwazo ili kuyapigisha magoti mataifa yasiyokubali kuburuzwa na mabeberu hao.

Tags