Araghchi atoa onyo kali kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni Asia Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i117054-araghchi_atoa_onyo_kali_kuhusu_jinai_za_utawala_wa_kizayuni_asia_magharibi
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Abbas Araghchi, ameeleza kuwa, jinai za utawala wa Kizayuni ndio chanzo cha mgogoro mkubwa katika eneo la Magharibi mwa Asia.
(last modified 2024-10-03T04:42:14+00:00 )
Oct 03, 2024 04:42 UTC
  • Araghchi atoa onyo kali kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni Asia Magharibi

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Abbas Araghchi, ameeleza kuwa, jinai za utawala wa Kizayuni ndio chanzo cha mgogoro mkubwa katika eneo la Magharibi mwa Asia.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametoa taarifa hiyo katika mkesha wa Mkutano wa 57 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na kuutaja ukatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni mifano ya kutisha ya ukiukwaji wa kimfumo na wa makusudi wa haki za binadamu, sheria za kimataifa na ni uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina.

Araghchi: Operesheni ya makombora ya SEPAH dhidi ya Israel ilikuwa ya kujihami 

Taarifa hiyo imesema, jinai za utawala wa Kizayuni ni dhihirisho baya la kampeni ya kimfumo ya ukiukaji wa haki za binadamu na sheria za kimataifa, na kuongeza kuwa, kinga isiyo na mipaka kwa utawala huo ghasibu wa Israel inasababisha maafa makubwa zaidi ya binadamu katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Palestina).

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesisitiza kuwa, walimwengu hawawezi kunyamaza kimya mbele ya jinai za utawala wa Kizayuni, na kuongeza kuwa, Tehran inatarajia Kamishna Mkuu na Baraza la Haki za Binadamu watalaani vikali jinai hizo.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesisitiza kuwa, jamii ya kimataifa inapaswa kuwafungulia mashtaka wahusika na washirika wote wa jinai hizo za kinyama katika mahakama za kimataifa na kitaifa na kuutisha mauaji ya utawala wa Kizayuni huko Gaza, Rafah, Lebanon na kote Asia Magharibi.