Kiongozi wa Mapinduzi: Adhabu uliyopewa utawala wa Kizayuni na vikosi vya ulinzi vya Iran ilikuwa halali na ya kisheria
(last modified Fri, 04 Oct 2024 12:21:24 GMT )
Oct 04, 2024 12:21 UTC
  • Kiongozi wa Mapinduzi: Adhabu uliyopewa utawala wa Kizayuni na vikosi vya ulinzi vya Iran ilikuwa halali na ya kisheria

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema katika khutba za Sala ya Ijumaa ya leo kwamba, kwa kuzingatia kanuni za kiulinzi za Uislamu, Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu na sheria za kimataifa, kazi adhimu na ya kiustadi iliyofanywa na vikosi vya ulinzi vya Iran ya kuuadhibu utawala mnyonyaji damu wa Kizayuni ilikuwa halali kabisa na ya kisheria.

Akihutubia umati adhimu na mkubwa mno wa wananchi katika ibada ya kiroho na kisiasa ya Sala ya Ijumaa mjini Tehran, Ayatullah Khamenei ameutaja umoja na mshikamano wa Waislamu kuwa ndio utakaowafanya wapate rehema na utukufu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ushindi dhidi ya maadui zao na akasisitiza kuwa: kwa kuzingatia kanuni za kiulinzi za Uislamu, Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu na sheria za kimataifa, kazi adhimu na ya kiustadi iliyofanywa na vikosi vya ulinzi vya Iran ya kuuadhibu utawala mnyonyaji damu wa Kizayuni ilikuwa halali kabisa na ya kisheria, na Jamhuri ya Kiislamu itatekeleza kwa nguvu, umadhubuti na uwezo kamili jukumu lolote itakalohisi kuwa nalo bila kusita wala kufanya pupa.
Umati wa waumini waliohudhuria Sala ya Ijumaa ya kihistoria ya Tehran

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria sera tofauti za kijeshi, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni za maadui zinazolenga kuleta migawanyiko na akasema: adui wa taifa la Iran ni adui wa mataifa ya Palestina, Lebanon, Misri, Syria, Iraq, Yemen na nchi zingine za Kiislamu na amri zote za kufanya hujuma na kuibua mifarakano zinatolewa kwenye kituo kimoja cha maagizo; na tofauti pekee iliyopo ni mbinu zinazotafautiana zinazotumiwa katika nchi za Kiislamu.

Ayatullah Khamenei amesisitiza kwa kusema: "inatulazimu kufunga mkanda kwa umadhubuti kwa ajili ya ulinzi, uhuru na heshima kuanzia Afghanistan hadi Yemen na kutoka Iran hadi Ghaza na Lebanon katika nchi zote za Kiislamu."
Katika khutba ya pili ya Sala ya Ijumaa aliyoisoma kwa lugha ya Kiarabu, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ameuhutubu Umma wote wa Kiislamu duniani na hasahasa mataifa azizi ya Lebanon na Palestina na akasema, shakhsia halisi ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, roho yake, njia na sauti yake angavu vitadumu milele.
Ayatullah Khamenei akihutubia waumini katika Sala ya Ijumaa ya Tehhran

Ayatullah Khamenei amesema, kushindwa adui muovu kuisababishia madhara makubwa taasisi imara ya Hizbullah, Hamas, Jihadul-Islami na harakati nyinginezo za Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu ndio sababu ya vitendo vyake vya mauaji, uharibifu, uripuaji na mauaji ya raia na kuwaumiza kwa mateso na majonzi raia wasio na silaha na akasema: "adui anavichukulia vitendo hivi kuwa ni alama ya ushindi kwake, lakini matokeo ya mwenendo huu ni kufutwa uwepo wake wa kuaibisha katika uga wa historia".

Aidha amesisitiza kuwa: kipigo chochote kitakachotolewa dhidi ya utawala wa Kizayuni na mtu yeyote na kundi lolote kunalihudumia eneo zima na wanadamu wote.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameielezea pia njozi ya Kizayuni na Kimarekani ya kudhamini uwepo wa utawala ghasibu wa Israel kuwa ni dhana potofu isiyowezekana kuthibiti na akasema: "utawala huu bandia ni mfano wa mti muovu ambao umeweza kujikongoja kwa tabu kwa kukokotwa na Marekani, na hili nalo kwa rehma za Mwenyezi Mungu halitadumu kwa muda mrefu".
Wananchi Waislamu wa Iran wakimuenzi Sayyid wa Muqawama, Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah

Ayatullah Khamenei amesema, genge la wahalifu la Kizayuni limeanza kufikia hatua kwa hatua hitimisho kwamba, kamwe halitaweza kuzishinda Hamas na Hizbullah, na akawahutubu wananchi wanamuqawama wa Lebanon na Palestina, wapiganaji shupavu na watu wao wenye subira na ushukurivu ya kwamba: "mauaji haya ya kufa shahidi na damu hii inayomwagwa havitadhoofisha vuguvugu lenu bali vitalifanya liwe imara zaidi".

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, Muqawama wa Ghaza umewashangaza walimwengu na kuupa heshima Uislamu na akasema, operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa na Muqawama wa mwaka mzima wa Ghaza na Lebanon vimeufanya utawala wa Kizayuni uingiwe na wahka na kiwewe cha kulinda uwepo wake; na akaongeza kuwa: "hii maana yake ni kwamba mapambano ya Jihadi ya wananchi wapiganaji wa Palestina na Lebanon yameweza kuurudisha miaka 70 nyuma utawala wa Kizayuni.../