Mkuu wa IRGC: Lebanon imepata 'ushindi wa kimkakati, na Israel imembulia fedheha
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) ameipongeza Lebanon na harakati yake ya Muqawama, Hizbullah kwa kufanikiwa kusimamisha vita vya Israel, na kuutaja kuwa ni "ushindi wa kimkakati kwa Hizbullah na wa kufedhehesha" kwa utawala ghasibu wa Israel.
Meja Jenerali Hossein Salami ameyasema hayo katika ujumbe aliotumwa kwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sheikh Naim Qassem leo Alkhamisi, siku moja baada ya kuanza kuutekelezwa makubaliano ya kusitisha vita kati ya Israel na Hizbullah kufuatia mapigano ya zaidi ya miezi 14.
"Katika upande wa Lebanon, Usitishaji vita ni kushindwa kistratijia na kufedhehesha kwa utawala wa Kizayuni, ambao haukuweza hata kukaribia malengo yake maovu katika vita dhidi ya Hizbullah," amesema Meja Jenerali Salam.
Ameongeza kuwa: Usitishaji huo wa mapigano "unaweza hata kuashiria mwanzo wa usitishaji mapigano na kumaliza vita dhidi ya Gaza."
Salami amebainisha kuwa, Israel imekubali kusitisha vita huko ikiwa chini ya msururu wa makombora ya Hizbullah yaliyokuwa yakilenga kambi na maeneo ya kistratijia ya utawala huo, na kwamba suala hilo linatoa somo kwa Tel Aviv na waungaji mkono wake.