Mkutano wa mawaziri wa nchi zinazouza gesi duniani waanza Tehran
Mkutano wa 26 wa nchi zinazouza gesi duniani umeanza shughuli zake hapa mjini Tehran.
Mohsen Paknejad Waziri wa Mafuta wa Iran amesema leo katika mahojiano na waandishi wa habari kwamba mkutano wa GRCF mjini Tehran unachunguza masuala mbalimbali katika nyanja ya biashara ya gesi na suala la kuzidisha kiwango cha uzalishaji.
Paknejad ameongeza kuwa, Mawaziri wa Nishati wa nchi wauzaji wakuu wa gesi duniani ambazo zina akiba kubwa ya gesi wanashiriki katika mkutano huu wa siku mbili hapa Tehran. Aidha Nchi nane wanachama watazamaji na na Oman pia zinashiriki katika mkutano huo.
Sayyd Ali Muhammad Mousavi Naibu Waziri wa Mafuta wa Iran anayehusika na masuala ya kimataifa pia amesema kuhusu mkutano huo kwamba: Nchi wanachama zina asilimi 70 ya akiba ya gesi, huku asilimia 40 ya mauzo yao ya gesi yakifanyika kupitia mabomba na asilimia 51 ya mauzo yake ya LNG.
Amesema ajenda muhimu ya vikao vya mawaziri ni kupasisha programu na bajeti, kumchagua Katibu Mkuu, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa kikao cha mawaziri na kuchunguza ada za wanachama.