Rais wa Iran awapongeza wananchi wa Gaza kwa ushindi dhidi ya Israel
-
Rais Masoud Pezeshkian
Rais Masoud Pezeshkian wa Iran leo Jumatatu amewapongeza wananchi wa Ukanda wa Gaza kwa ushindi wao katika kukabiliana na vita vya kikatili na mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel yaliyoendelea kwa miezi 15.
Rais wa Iran amesema kuwa wananchi wa Gaza wameyafunza mataifa mengine namna ya kusimama kidete dhidi ya ugaidi.
Rais Masoud Pezeshkian ameeleza haya baada ya kuanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas).
Makubaliano haya yamefikiwa baada ya utawala wa Israel kusalimu amri mkabala wa oparesheni zilifanikiwa za makundi ya mapambano ya ukombozi dhidi ya Israel.
Rais wa Iran ameashiria mauaji ya kimbari yaliyofanywa na Israel na waungaji wake mkono ndani ya eneo dogo la kijiografia la Gaza na kuwauwa shahidi Wapalestina karibu 47,000 aghalabu yao wakiwa wanawake na watoto na kuyataja kuwa ni mfano wa wazi wa ugaidi.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Rais Pezeshkian ameitaja Iran kuwa ni mhanga wa ugaidi na kuashiria namna maadui walivyotekeleza mauaji dhidi ya raia wa Iran wakiwemo maafisa wa serikali, shakhsia watajika na wasomi mbalimbali tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu kama wenzo wa kukwamisha uustawi wa mapinduzi hayo.