Muqawama ndiyo njia pekee ya kupambana na Marekani
(last modified Fri, 24 Jan 2025 12:05:49 GMT )
Jan 24, 2025 12:05 UTC
  • Muqawama ndiyo njia pekee ya kupambana na Marekani

Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesisitiza kuwa, njia pekee ya kukabiliana na uadui na tamaa za kupindukia za Marekani ni kuendeleza Muqawama.

Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami, amesema hayo kwenye khutba za Sala ya Ijumaa ya leo ya hapa mjini Tehran na kusisitiza kwamba njia pekee ni kupambana jinai za kuchupa mipaka na kupenda makuu Marekani ni kufanya kama Ukanda wa Ghaza ambako Muqawama umeshinda licha ya kuweko njama zote hizo dhidi yake na ndio maana leo hii tunasherehekea kushindwa Marekani.

Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran ameongeza kuwa, walimwengu wanapaswa kujua kwamba msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu Marekani ni uleule msimamo wa Imam Khomeini (RA) na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Imam alisema, Marekani ni shetani mkubwa. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei naye amekuwa akisisitiza mara kwa mara kwamba Marekani ni shetani mkubwa. 

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameonya pia kuhusu hatari ya mamluki wanaojipenyeza na kuongeza kuwa Marekani hivi sasa inataka kufanya mazungumzo na Iran kama njia ya kuyapiga vita Mapinduzi ya Kiislamu.

Kuhusu usitishaji vita huko Ghaza, Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amebainisha kuwa: Usitishaji huo wa mapigano ni kushindwa kusiko na chembe ya shaka utawala wa Kizayuni na hilo linathibitishwa na wimbi la kujiuzulu viongozi wa Israel kutokana na kashfa walizopata kuanzia wakati wa Kiumbenga cha al Aqsa hadi hivi sasa. 

Ayatullah Khatami amezungumzia pia suala la kuingia madarakani utawala wa Donald Trump huko Marekani na kusema: "Kwa taifa la Iran, Warepublican na Wademokrat hawana tofauti yoyote. Kwa bahati mbaya, Marekani imefanya oparesheni za aibu mno dhidi ya taifa la Iran tangu wakati wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu."