Apr 26, 2024 12:07 UTC
  • Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Vikosi vya ulinzi vya Iran ni mihimili imara mno ya taifa

Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema: Vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mihimili imara mno kwa taifa na inayoiletea dini izza na heshima.

Ayatullah Seyed Ahmad Khatami, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran ameashiria operesheni ya Ahadi ya Kweli ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kuutia adabu utawala wa Kizayuni wa Israel na akabainisha kuwa: kisasi ulicholipiza Mfumo wa Kiislamu kwa utawala wa Kizayuni kilikuwa cha kumtia adabu mchokozi; na kama watataka kurudia kufanya upuuzi mwingine watachapwa kibao kikali zaidi.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesema, katika operesheni hiyo, adui alielewa vyema kwamba nara na kaulimbiu za Iran zinaandamana na vitendo na akaongeza kuwa: katika operesheni hiyo, vikosi vya ulinzi vya Iran vililenga vituo vilivyotumika kufanyia shambulio dhidi ya sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran tu mjini Damascus; na hatua hiyo imedhihirisha jinsi Iran inavyofanya mambo kwa busara na mantiki.

 
Katika sehemu nyingine ya hotuba za Sala hiyo, Ayatullah Khatami amesema: "tumeshuhudia jinai za kinyama za Wazayuni na nguvu za kambi ya Muqawama katika matukio ya Ghaza", na akaongeza kuwa: umati wa wanachuo wa Marekani katika chuo kikuu cha California na nchini Ufaransa umejitokeza kuwaunga mkono wanaodhulumiwa, lakini nchi inayojigamba kiunafiki kuwa mtetezi wa haki za binadamu imewatia nguvuni watu 100 miongoni mwa wanachuo na walalamikaji hao.../

 

Tags