Mabadilishano ya kibiashara ya Iran na nchi jirani yaongezeka
Mabadilishano ya kibiashara ya Iran na nchi jirani yanaonekana kuongezeka katika miezi michache ya hivi karibuni.
Mabadilishano ya kibiashara ya Iran na nchi jirani yalifikia takriban dola bilioni 60 katika miezi 10 ya mwaka huu, ambayo ni ongezeko la 19% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Msemaji wa Kamisheni ya Maendeleo ya Biashara ya Khane Samt amesema: Katika miezi 10 ya mwaka huu, zaidi ya tani milioni 93.5 za bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 59.7 zilibadilishwa kati ya Iran na nchi 15 jirani, ambazo ziliongezeka kwa 16.2% ya uzito na 19.2% ya thamani ikilinganishwa na kipindi hicho mwaka uliopita.
Kuhusu biashara isiyo ya mafuta ya Iran na nchi jirani, Seyed Ruhollah Latifi alisema: Tangu mwanzoni mwa mwaka hadi mwisho wa Januari, tani 93,566,462 za bidhaa zisizo za mafuta zenye thamani ya dola bilioni 59,656,707,995 zilibadilishwa kati ya Iran na nchi 15 jirani.
Ushirikiano na majirani daima umekuwa ndio kipaumbele cha siasa za nje za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika miaka ya hivi karibun. Katika muktadha huo, harakati za kutafuta njia za kupanua ushirikiano wa pande mbili zimekuwa ndio lengo kuu la viongozi wa Iran na nchi jirani.
Kujikita wauzaji bidhaa wa Iran katika masoko ya kieneo pia kumeongeza mauzo ya bidhaa nje, na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina nafasi muhimu na ya kimsingi katika kukidhi mahitaji ya kiuchumi ya nchi jirani. Makampuni ya Iran pia yamewekeza katika miradi mikubwa ya miundombinu nje ya mipaka ya nchi.