Iran yachunguza barua ya Rais wa Marekani
(last modified Fri, 14 Mar 2025 02:46:24 GMT )
Mar 14, 2025 02:46 UTC
  • Iran yachunguza barua ya Rais wa Marekani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa baada ya tathmini na uchunguzi kamili wa barua ya Rais wa Marekani kwa Iran, uamuzi utachukuliwa kuhusu jinsi ya kujibu barua hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari IRNA, Ismail Baghaei Hamaneh, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, amesema kuwa barua hiyo ilipokelewa Jumatano usiku na kwa sasa inachunguzwa.

Baghaei ameongeza kuwa, baada ya tathmini na uchambuzi wa kina, uamuzi utafanywa kuhusu namna ya kujibu barua hiyo.

Anwar Gargash mshauri wa kidiplomasia wa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu  (UAE), siku ya Jumatano alikabidhi barua hiyo kutoka kwa Rais wa Marekani kwa Seyed Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran.

Mnamo Ijumaa, Machi 7, Donald Trump alitangaza katika mahojiano na Televisheni ya Fox Business kuwa alikuwa amemtumia barua Kiongozi Muadhamu wa Iran.